Kuukoseha mwili mazoezi kunasababisha vifo vya mapema
Je ulijua kama watu wengi barani Ulaya wanakufa kwa kukosa
kufanya mazoezi ikilinganishwa na idadi ya watu wanaokufa kutokana na ugonjwa
wa kisukari au ?
Kwamba ukosefu wa mazoezi unaua mara mbili ikilinagishwa na
ugonja wa kisukari? Basi ikiwa ulikuwa huna habari , habari ndio hiyo.
Watafiti waligundua hili kutokana na utafiti wao walioufanya
kwa mwaka mmoja kuwachunguza watu 300,000.
Watafiti kutoka chuo kikuu cha Cambridge walisema kwamba
vifo 676,000 vinavyoripotiwa kila mwaka vinatokana na watu kukosa mazoezi
ikilinganishwa na vifo 337,000 vinavyotokana na uzito au unene wa kupindukia.
Walisema kwamba ikiwa watu wataamua kutembea tu kwa dakika
20 kila siku itakuwa na manufaa makubwa sana kwa mwili.
Wataalamu wanasema mazoezi yana manufaa sana kwa watu wenye
uzani wowote ule.
Mojawapo ya sababu za watu kunenepa kupita kiasi au
'Obesity' huwa ni kukosa mazoezi.
Hata hivyo, inajuikana kwamba watu wanaokuwa wembamba pia
kupita kiasi wanakabiliwa na changamoto nyingi za kiafya ikiwa pia watakosa
kufanyisha mwili mazoezi.
Na pia watu wanene kupita kiasi ambao hufanya mazoezi
wanakuwa katika hali nzuri ya kiafya.
Utafiti huo, ulilenga kuonyesha athari za kukosesha mwili
mazoezi.
Baadhi ya magonjwa yanayowaandama watu wanokosa kufanya
mazoezi ni pamoja na maradhi ya moyo ingawa kisukari ndio ugonjwa ambao watu
wanene sana wako katika hatari ya kuugua.,
No comments:
Post a Comment