Sio kawaida kwa ziara alizopangiwa Rais wa Korea Kaskazini
kutangazwa hadharanbi kabla ya safari
Serikali ya Urusi inasema kwamba Rais wa Korea Kaskazini
amekubali mwaliko wa Rais wa nchi hio kuzuru Urusi.
Taarifa hii ni ka mujibu wa shirika la habari la Yonhap nchini
humo.
Shirika hilo la habari limenukuu ujumbe kutoka kwa ikulu ya
Urusi, Kremlin ingawa taarifa hio haijamtaja rasmi Kim Jong-un.
Hata hivyo Yonhap linamnukuu afisa mmoja wa wizara akisema
kumtaja kiongozi huyo haina umuhimu wowote.
Kim Jong-un hajafanya ziara katika nchi za kigeni tangu
kuchukua mamlaka mwaka 2011.
Kituo chake cha kwanza kitaangaliwa kwa karibu sana kwa
sababu ya kile wnegi wanasema ni sera zake kanadmizi.
Mapema mwezi huu, taarifa zilisema kwamba Urusi ndio itakuwa
nchi ya kwanza kumwalika Rais Kim.
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov aliambia
wandishi wa habari kuwa mnamo tarehe 21 mwezi Januari, Rais Kim atapewa mwaliko
wa kwenda Urusi kwa sherehe za kuadhimisha mwisho wa vita vya pili vya dunia
zitakazofanyika tarehe 9 mwezi Mei.
Alisema kuwa dalili ya kwanza kutoka kwa serikali ya Korea
Kaskazini inaonyesha mambo yako shwari.
Shirika la habari la Yonhap lilisema kuwa majibu wa taarifa
kutoka kwa ofisi ya Rais wa Urusi, Rais wa Korea Kaskazini ni mmoja wa viongozi
walioalikwa kutoka nchi 20 na ambao wamethibitisha kuhudhuria sherehe hizo.
Lakini barua hiyo haikuthibitisha ikiwa Rais Kim ni mmoja wa
walioalikwa wala ikiwa amekubali mwalikoi huo kwani ilisema: ''Orodha ya
watakaohudhuria haijakamilishwa, tunaendelea na mikakati ya kuthibitisha
wakaohudhuria
Hapajakuwa na taarifa rasmi kutoka kwa serikali ya Korea
Kaskazini kuhusu tetesi hizo.
Kim Yong-nam, ambaye kikatiba ni Rais asiye na mamlaka wa
nchi hio ndiye amekuwa akiwakilisha Korea Kaskazini katika mikutano katika nchi
za kigeni.
Ziara za marehemu babake Rais Kim, Kim Jong-il, hazikuwa
zikitangazwa hadharani kabla ya yeye kuondoka nchini humo.
No comments:
Post a Comment