Kocha wa Southampton, Ronald Koeman ana wasiwasi kuwa huenda
Victor Wanyama akakosa kucheza kwa hadi wiki tano baada ya kuumia msuli wa paja
katika mechi ya Kombe la FA dhidi ya Ipswich.
Wanyama alitolewa muda mfupi kabla ya mapumziko, katika
mechi ambayo Southampton walishinda 1-0.
Koeman, ambaye amesema mechi za marudiano, katika kipindi
hiki chenye mechi nyingi ni "wazimu", alikuwa amepanga kumchezesha
Wanyama kwa dakika 45 tu.
"Tuna majeruhi wengine tayari. Kama ni msuli wa paja,
basi itakuwa wiki nne au tano." amesema Koeman.
Wanyama, ambaye ni mchezaji wa kimataifa kutoka Kenya amekuwa
mchezaji muhimu kwa Southampton msimu huu, akicheza mechi 24.
No comments:
Post a Comment