Wanahabari wakimsikiliza Kamishna Kova (hayupo pichani)
KAMISHNA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar e s Salaam, Suleiman
Kova ametoa tamko mbele ya wanahabari juu ya maandamano ya vijana wa Chama
cha Wananchi CUF (JUVICUF) yaliyokuwa yamepangwa kufanyika Leo.
Kamanda Kova amewataka vijana wa CUF kutoandamana leo na kama wataandamana jeshi hilo halitakuwa tayari kuona maandamano
hayo yakifanyika .
Alisema kuwa maandamano hayo yalikuwa yamepangwa kufanyika leo Februari 13 mwaka huu
kutoka Buguruni, Shule ya Uhuru, Mnazi Mmoja, Mtaa
wa Ohio hadi Tume ya Taifa ya Uchaguzi
na kisha Wizara ya Mambo ya Ndani ,kwa dhumuni la kuitaka Tume ya Taifa
ya Uchanguzi (NEC) iongeze siku za uandikishwaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura kutoka siku saba hadi siku 14, pamoja na kulaani ukiukwaji wa haki za
binadamu unaofanywa na jeshi la polisi nchini.
Kova ametaja sababu za kuzuia maandamano hayo kuwa siku
waliyoomba ni siku ya kazi, ambapo maandamano hayo yakifanyika yatasumbua mfumo
mzima wa shughuli za jiji zima, kibiashara, huduma za afya, walemavu, watoto na
n.k.
(Habari/Picha:
Gabriel Ng’osha/GPL)
No comments:
Post a Comment