Kijana Mussa akiwa hoi baada ya kung'olewa meno. |
Kijana aliyefahamika kwa jina moja la Musa hivi karibuni
alichezea kichapo cha nguvu kisha kung’olewa meno kwa koleo baada ya kunaswa
akitaka kuiba nyumbani kwa mtu.
Tukio hilo lilitokea katika mji mdogo wa Tunduma uliopo
wilayani Momba mkoani hapa ambapo kijana huyo alinaswa akiingia kwenye nyumba
iliyopo Mtaa wa Tazara, Kata ya Kaloleni ya mtu aliyefahamika kwa jina la
Mahinya.
Chanzo cha kuaminika kilichoomba hifadhi ya jina lake
kilieleza: “Yule jamaa alionekana mara ya kwanza akiingia kwenye nyumba ya
Mahinya, aliposhtukiwa akakimbia.“Kama vile haitoshi mida ya saa 10.30 jioni
akarudi tena akitaka kuiba na ndipo watu walipomkamata na kumpa kipigo
Akiwa mikononi mwa polisi.
“Akaminywa sehemu za siri kisha akang’olewa meno kwa koleo
na baadaye akapelekwa Kituo Kidogo cha Polisi Tunduma kwa hatua za kisheria
lakini akiwa nyang’anyang’a.”CHANZO GPL
No comments:
Post a Comment