Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, February 22, 2015

Mbeya City wakesha kulinda Sokoine


Mbeya. Katika kile kinachoonekana kutokuwa na imani na watu waliojitokeza katika mchezo wa juzi kati ya Prisons na Yanga, baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa ni mashabiki wa Mbeya City, waliingia lindoni baada ya mchezo huo ili kulinda Uwanja wa Sokoine usiharibiwe.
Watu hao ambao walionekana kutokuwa na imani na kila mtu aliyekuwa akikatiza katika nyasi za uwanja huo, walikuwa wakali hata kwa shabiki maarufu wa Yanga anayetumia staili ya kujipaka masizi usoni na kujaza nguo nyingi tumboni.


Gazeti hili lilishuhudia watu hao baada ya mahojiano ya makocha wa Prisons na Yanga wakikataza watu kupitia hata kando ya uwanja huo kwa kudai kuwa kuna imani za kishirikina.
Mmoja wa watu hao waliokuwa wakizuia watu bila kutaja jina lake, aliliambia gazeti hili kuwa Yanga imefika Mbeya ikiwa na watu wengi ,wakiwamo wazee wa klabu hiyo na hawatakubali kuchezewa akili katika uwanja wao.
“Tupo hapa kwa ajili ya kuhakikisha uwanja hauharibiwi kwa chochote, iwe imani za kishirikina au kwa njia nyingine, wenzetu wamefungwa hapa na hatutaki na sisi kupoteza mchezo,” alisema mtu huyo aliyekataa kutaja jina lake.
Aliongeza kuwa timu zao msimu huu ziko katika nafasi mbaya na wanahofia zote kupoteza michezo hiyo miwili dhidi ya Yanga

No comments:

Post a Comment