Morocco imepinga vikwazo ilivyowekewa na Shirikisho la
Kandanda barani Afrika, Caf kwa kushindwa kuandaa michuano ya Kombe la Mataifa
ya Afrika ya mwaka 2015.
Caf imeipiga marufuku Morocco kushiriki michuano miwili
ijayo ya Caf, wakati huo huo ikikipiga faini chama cha mpira wa miguu cha nchi
hiyo dola za Kimarekani milioni moja na kutaka fidia ya euro milioni nane, sawa
na pauni za Uingereza milioni £5.9 kutokana na hasara iliyopatikana kwa nchi
hiyo kushindwa kuandaa mashindano hayo.
Shirikisho la soka la Morocco, FRMF limesema "linapinga
vikwazo vyote vya michezo na fedha".
Chama hicho kimesema kinaamini "hakuna msingi wa
kisheria" kwa adhabu hizo.
Fainali za Afcon za mwaka 2015 zilizomalizika Jumapili,
zilihamishiwa Equatorial Guinea baada ya Caf kukataa ombi la Morocco la
kuahirisha fainali hizo kwa hofu ya ugonjwa wa Ebola, ambao uliyaathiri kwa
kiasi kikubwa mataifa ya Afrika Magharibi ambako timu nyingi zilizofuzu kucheza
fainali hizo zinatoka.
FMRF imesema katika mtandao wake: "kamati ya utendaji
inasemekana kushtushwa sana na maamuzi yaliyochukuliwa na Caf.
"hayaendana kwa namna yoyote na hitimisho lililofikiwa
katika mkutano wa kwanza na rais wa Caf, mjini Cairo, Misri."
Baada ya mkutano huo wa Januari na rais wa Caf, Issa
Hayatou, rais wa shirikisho la mpira wa miguu la Morocco, Faouzi Lakjaa,
amesema adhabu itakuwa tu ya fedha.
FRMF imesema kuwa"chukua hatua zote muhimu za kuunga
mkono na maslahi ya mpira wa miguu wa Morocco".
No comments:
Post a Comment