Hali ya hewani kuchafuka Bungeni hii Duniani kote iko,
ukiyaona leo Bongo sio mageni, kuna wakati utayaona hayo hata kwenye Mijengo ya
Mabunge ya wenzetu yaani.
Leo kubwa iliyokaa kwenye kurasa za mbele Magazetini,
mitandaoni, ishu ya Wabunge wa upinzani Afrika Kusini kumkatisha Rais Zuma
wakati akihutubia Bungeni jana jioni FEBRUARY 12 na kuanzisha mzozo mkubwa
wakimtaka Rais huyo aeleze kuhusu tuhuma za Rushwa na Ufisadi zinazomkabili.
“Tunamtaka Rais atujibu majibu mepesi; lini atarudisha pesa
zetu“– alihoji Mbunge wa Upinzani, Julius Malema.
Julius Malema akiongea na waandishi wa habari baada ya
kutolewa Bungeni.
Spika wa Bunge Baleka Mbete alimtaka Malema kutoka nje
ambapo baada ya kuonekana akibisha kundi la askari walivamia na kumtoa kwa
nguvu ndani ya Jengo hilo pamoja na baadhi ya Wabunge, ambapo baadaye Rais Zuma
aliendelea na hotuba yake.
Mwezi Novemba 2014 Mbunge Mashabela aliwahi kutamka ndani ya
Bunge hilo kuwa Rais Zuma ni mwizi hali ambayo ilichafua pia hali ya hewa
kwenye Bunge hilo kwa kiasi kikubwa.
Hii ni video ya tukio la mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment