Pages

Thursday, March 26, 2015

ANGALIA KITUKO THIERY HENRY ALICHOWAFANYIA WANAFUNZI

Mkongwe wa soka wa zamani wa klabu ya Arsenal Thierry Henry aligeuka kichekesho baada ya kuwasuprise wanafunzi wa shule ya Pen-Y-Dre ya nchini Wales.Henry aliingia darasa la wanafunzi hao na kuzuga kama mwalimu ambapo aliingia na kujitambulisha kisha kumpa tuzo mwanafunzi Emma Morgan ambaye ni mdogo kiumri aliyeshinda tuzo ya kuogelea huku akiwa amevalia wigi na miwani.
Haikuwa rahisi wanafunzi hao kufahamu kama ni yeye kutokana na wigi la kike alilokuwa amevaa pamoja na miwani vitu ambayo viliwachanganya na kushindwa kumwelewa.

 

Henry kwa sasa ni mtangazaji katika kituo cha Televisheni cha Sky Sports News akiwa kama mchambuzi wa soka kipindi ambacho hurushwa jumapili na alikwenda shuleni hapo kwa ajili ya ya kutoa tuzo hiyo.
Maandishi na Millard ayo

No comments:

Post a Comment