Dah! hii hatari sana. kijana mmoja wa bodaboda maeneo ya
Sinza Afrikasana jijini DSM ambaye jina halikupatikana, alikoswakoswa kuuawa
baada ya kupora mkoba uliokuwa na simu ya mwanamke aliyekuwa akipita njia. Cha
ajabu kijana huyo alivyokwapua mkoba, pikipiki iligoma kuwaka basi raia wenye
hasira kali wakaanza kumshushia kipigo
kikali. Kijana aliponea chupuchupu
kuchomwa moto,
kwani waliokuwa wamefuata mafuta ya petroli waliporudi walimkuta
trafiki akizuia asiuawe basi raia hao walihamishia hasira zao kwenye kuichoma
moto bodaboda ya kijana huyo.chanzo EaTV
No comments:
Post a Comment