Msanii wa Bongo Fleva,Khadija Shabani’Keisha’ amenusurika kifo baada ya kupata ajali maeneo ya Maktaba, Posta jijini Dar.
Akizungumza na Clouds Fm alisema kuwa
alikuwa akitoka chuoni CBE na kwamba alikuwa akimfuata mumewe alipofika
maeneo hayo ndipo lilipotokea gari na kumuovateki na kuligonga gari
lake. Aidha
alisema kuwa alisikia maumivu na alipokwenda hospitali kufanyiwa vipimo vilionyesha hakupata majeraha kwa ndani.
alisema kuwa alisikia maumivu na alipokwenda hospitali kufanyiwa vipimo vilionyesha hakupata majeraha kwa ndani.
“Nashukuru Mungu nilipimwa
hospitali vipimo vilionyesha sikupata madhara yoyote kwa ndani kwani
nilikuwa na wasiwasi labda niliumia kwa ndani,” alisema Keisha.
Source: http://www.cloudsfm.co/
No comments:
Post a Comment