Rais anayeondoka madarakani nchini Namibia Hifikepunye
Pohamba, 79,ameshinda tuzo ya dola milioni tano ya Mo Ibrahimu ya uongozi wa
Afrika.
Tuzo hiyo ya dola milioni 5 hutuzwa kiongozi wa Kiafrika
aliyechaguliwa na anayeongoza kwa njia bora na kuinua maisha ya watu na
kuondoka ofisini
Bwana Pohamba ambaye anaondoka madarakani baadaye mwezi huu
ndiye mwanzilishi wa kundi la SWAPO lililopigania uhuru wa Namibia.
Rais huyo anatarajiwa kumkabidhi madaraka rais mteule Hage
Geingob.
Pohamba amehudumu vipindi wili kama rais wa Namibia alipo
chaguliwa kwanza mwaka wa 2004 na tena mwaka wa 2009.
Mwanabiashara raia wa Sudan Mo Ibrahim ndiye alizindua tuzo
hilo kuwapa motisha viongozi wa Afrika kuondoka madarakani kwa njia ya amani.
Rais anayeondoka madarakani nchini Namibia Hifikepunye
Pohamba, 79,ameshinda tuzo la dola milioni tano la Mo Irahimu la uongozi wa
Afrika.
Aliyekuwa rais wa Msumbiji Joaquim Chissano ndiye aliyetuzwa
kwanza mwaka wa 2007na ndiye alichangia pakubwa kwa kujaribu kutafuta uwiano
baina ya viongozi kadhaa barani Afrika
Mmoja wa wanajopo wanaoteua marais wanaopewa tuzo hilo Salim
Ahmed Salim amemtaja Pohamba kama mtu aliyeiunua maisha ya watu wake
Mshindi anapokea dola milioni 5 ambayo huwa inagawanywa
ilikutolewa katika kipindi cha muongo mmoja kisha washindi wanatuzwa dola
lakimi mbili kila mwaka hadi siku ya kufa.
No comments:
Post a Comment