Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Urusi Sergey Lavrov
akiwasili Geneva
Waziri wa mashauri ya kigeni wa marekani John Kerry ameonya
Urusi akisema kuwa itawekewa vikwazo zaidi ikiwa makubaliano ya kusitisha
mapigano mashariki mwa Ukrain hayatatekelezwa kilamilifu.
Kerry aliyasema hayo mjini Geneva baada ya kufanya
mazungumzo na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov.
Bwana Kerry alisema kuwa waasi wanaondoa silaha nzito kutoka
sehemu fulani tu ambapo pia
wamekataa kuwaruhusu waangalizi wa kimataifa
kuingia eneo hilo ili kujionea wenyewe jinsi hali ilivyo.
Kerry amesema kuwa ikiwa hali hiyo itaendelea kutakuwa na
vikwazo zaidi dhidi ya Urusi ambayo tayari uchumi wake uko katika hali mbaya.
Hata hivyo kerry amesema ana matumaini kuwa mazungumzo na
mwenzake wa Urusi yataleta sulUhu na kumaliza mapigano nchini Ukrain.
Bwana Lavrov pia alizungumzia umuhimu wa kutekelezwa kwa
makubaliano ya Minsk lakini pia amesema kuwa kuna maendelea na huenda mapigano
hayo yakasitiswa
Mkutano huo vilevile unasadifiana na kutolewa kwa ripoti
maalum ya Umoja wa mataifa inayoshtumu vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu
mashariki mwa Ukraine.
UN inasema kuwa zaidi ya watu 6000 wameuawa tangu mapigano
hayo yaanze huku mamia wakiuawa katika majuma machache yaliyopita.
Bwana Kerry anatarajia kuzua mjadala kuhusiana na mauaji ya
kiongozi wa upinzani ambaye pia ni mpinzani sugu wa rais Putin Boris Nemtsov.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Urusi Sergey Lavrov
akiwasili Geneva
Kiongozi huyo alipigwa risasi na kuuawa karibu na makao
makuu ya urais wa urusi Kremlin siku ya ijumaa iliyopita.
Huku hayo yakijiri, Tume ya jumuia ya Bara Ulaya inatazamia
kufanya mazungumzo kati ya Moscow na Kiev, ili kutazua tatizo lililoko
kuhusiana na usambazaji wa gesi.
Juma lililopita kampuni kubwa ya uuzaji gesi, Gazprom,
liliwaonya wasambazaji wake kuwa itakomesha pakubwa uuzaji wake wa gesi nchini
Ukraine hadi Ukraine kutuma malipo yake ya gesi mwezi huu wa Machi.
Aidha mataifa hayo mawili yanatofautiana kuhusiana na
usambazaji wa awali wa gesi kwa makundi ya wapiganaji mashariki mwa Ukraine.
Mwezi uliopita, Kiev ilisimamisha kutuma gesi hadi katika
maeneo yaliyojitenga, ikidai kuwa mabomba ya kupitishia mafuta na gesi
yameharibiwa huku kampuni ya Gazprom ikiwasambazia waasi mafuta moja kwa moja.
No comments:
Post a Comment