Msanii wa Kundi la Orijino Komedi, Mujuni Sylivery aka Mpoki
moja ya vitu ambavyo aliwahi kuvifanya katika kazi yake ya uchekeshaji ni
pamoja na kuigiza sauti ya marehemu, Kapteni John KOMBA ambaye amefariki February 28.
Jana Mpoki amesikika kwenye Leo Tena @CloudsFM, alianza
kuzungumzia namna alivyopokea taarifa za msiba huo; “..Mtu akishatoweka kwenye
ulimwengu akifariki dunia inauma kwa sababu mtu unayempoteza leo huwezi kumpata
tena.. lakini ukimpoteza mbuzi utaenda Vingunguti
utamnunua na sherehe
itaendelea.. Kitendo cha kufariki mtu yoyote hata kama hajulikani ni pengo
kubwa tu”
“Imeniathiri kwa kisanii kwa kuwa nilikuwa namuwezea, kidogo
alikuwa hapendi lakini ilivyokuja akatulia.. Watu wakamwambia bwana hawa watoto
tu.. Ukimuiga mtu ana mazuri huwezi kumuiga kwa mabaya tu.. ana mazuri
yake..Ikanipa wigo mpana kwenye kazi yangu ya kubuni sauti yake, vitendo..“
“mwisho wa siku kaondoka pengo lake halitozibika.. Kama kuna
la kufanya kuhusu yeye kwa kumuenzi sitokuwa nyuma, nitafanya ili mradi
lisimvunjie heshima Marehemu, familia yake, jamii, viongozi wenzake Bungeni na
watu wote ambao kawaacha kwenye jimbo lake sasa hivi wapweke..“
No comments:
Post a Comment