TAARIFA KWA UMMA
Naomba nitumie nafasi hii kukanusha uongo ulioenezwa na
wahuni kuwa Katibu Mwenezi wa CCM Ndugu Nape Nnauye na Mwenyekiti wa CCM mkoa
wa Arusha Ndugu Onesmo Nangole walichapana makonde leo. Uongo huo umeandikwa
leo Machi 17, 2015 saa 16:34 PM na kusambazwa kwa mara ya kwanza kupitia
IP.21.372.11.7 katika tower namba 4.
Suala hilo ni uongo wa dhahili wenye malengo mahsusi ya
kuwachonganisha viongozi hao wawili
ambao kwa pamoja wanaendelea kufanya kazi nzuri
ya kuijenga CCM mkoani Arusha kupitia ziara ya Katibu mkuu wa CCM Abdulrahman
Kinana.
Mambo yakudhihirisha kuwa huo ni uongo ni kwamba leo wakati
uongo huo unaandikwa huku ukionesha kuwa vurugu na ugomvi huo umetokea katika
Hotel ya Naura Spring jijini Arusha, Viongozi wote hao wawili hawajafika kabisa
katika jiji hilo.
Kwani kwa wiki nzima wamekuwa katika wilaya za pembezoni za
mkoa wa Arusha yaani Monduli, Ngorongoro, Karatu na leo Longido ambapo mpaka
muda huu wanaendelea na mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Namanga mpakani
mwa Tanzania na Kenya.
Leo viongozi wote watalala hapa Longido mjini na wala sio
Arusha mjini kama uongo huo unavyosema.
Naomba watanzania puuzieni uongo huo ambao hauna mbele wala
nyuma.
Viongozi wote wawili yaani Ndugu Nape na Ndugu Onesmo
wameonesha ushirikiano mkubwa saana katika ziara ya katibu mkuu wa CCM
inayoendelea mkoani Arusha na wala hawajapishana kwa maneno na hata kunyosheana
kidole.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Umma
CCM Makao Makuu.
No comments:
Post a Comment