Mahakama moja mjini Busia, imewahukumu washukiwa watatu
vifungo vya kati ya miaka saba na kumi na tano gerezani,baada ya kuwapata na
hatia ya kumbaka na kumjeruhi msichana mmoja, aliyefahamika kama Liz.
Liz inasemekana alishambuliwa na vijana hao na kubakwa
wakati alipokuwa akirejea nyumbani kutoka kwa mazishi ya babu yake katika eneo
la Busia Magharibi mwa Kenya.
Tukio hilo lilizua mjadala mkali nchini Kenya huku
wanaharakati wa kijamii wakishinikiza serikai kuwachukulia washukiwa hao hatua
kali.
Watatu hao walikuwa wamehukumiwa ''kufyeka nyasi katika
kituo cha polisi'' na kuachiliwa huru.
Hata hivyo msichana huyo alikuwa amepooza kiwiliwili chake
kuanzia kiunoni kufuatia kutupwa katika shimo ilikuficha ushahidi alipata
msaada baada ya wanaharakati wa kupigania haki za
kibiniadamu kuishinikiza polisi kuchukua hatua dhidi ya polisi waliotoa hukumu
hiyo nyepesi dhidi ya watu hao watatu.
No comments:
Post a Comment