Askofu wa Kanisa la Baptist lililopo Kyela, mkoani Mbeya, Langeni Anyimike Mwasibira (40) amesena hali yake ni mbaya na anashindwa kuhubiri Neno la Mungu kutokana na maumivu makali anayoyapata baada ya kuugua ugonjwa wa ajabu uliosababisha uvimbe kutokea shavuni.
Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu wiki iliyopita akiwa kijiji kwao Kisyosyo, Kata ya Matema, Wilaya ya Kyela, Mbeya, askofu huyo
alisema kwamba kwa sasa hali aliyonayo haimpi matumaini ya kuendelea kuishi hapa duniani.
“Hali yangu ni mbaya sana, nawaomba Watanzania wanisaidie kunichangia shilingi milioni kumi na mbili kwa ajili ya matibabu na nauli ya kwenda India na kurudi.
“Madaktari wa Hospitali ya Muhimbili waliokuwa wakinihudumia wamenirudisha nyumbani sasa ni mara ya pili wakinieleza kwamba nisubiri kama Wizara ya Afya itanisafirisha kwenda India kutibiwa. Wamesema kama nina uwezo wa kujigharamia mwenyewe niwe na shilingi milioni 12.
“Nimeteseka na ugonjwa huu wa ajabu kwa muda wa miaka 27, sasa unanipeleka pabaya kwani hata familia ipo matesoni. Nina mke na watoto watano, walikuwa wakinitegemea lakini kwa sasa sina uwezo na mke wangu ndiyo anatusaidia kutokana na kilimo cha jembe la mkono.
“Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya mwaka 2,000 nilifika Muhimbili wakadai kwamba huenda ni kansa hivyo niende Ocean Road. Hata hinyo, walidai kwamba siyo na kunieleza nirudi Muhimbili, walifanya vipimo wakasema hawajabaini kitu na hawawezi kunifanyia upasuaji, nilikaa kwa muda wa miezi minne wakaniambia niende nyumbani nikapumzike, hamna jinsi ya kunisaidia, nikarudi nyumbani.
“Nikiwa nyumbani hali yangu ilizidi kuwa mbaya, mwaka 2007 niliomba fedha ya nauli ya kuja Muhimbili, madaktari walikata kipande cha nyama katika uvimbe walipoifanyia kipimo,walisema matibabu yangu na vipimo kamili ni mpaka India, hivyo nirudi nyumbani.
“Mwaka 2014 nikiwa kijijini hali ilikuwa mbaya sana, niliambiwa kuna daktari bingwa Kigoma, nilienda ambapo nilifanyiwa upasuaji nikiamini ningepona lakini hali ikawa tofauti, nilikaribia kufa, nikakimbizwa Muhimbili.
“Juni 18, mwaka jana madaktari wa Muhimbili waliiandikia barua Wizara ya Afya ili nipelekwe India, niliambiwa nirudi nyumbani kusubiri majibu toka wizarani lakini hadi leo hii (juzi) sijapata taarifa yoyote, hivyo naomba msaada,” alisema askofu huyo.
Kwa yeyote mwenye moyo wa huruma aliyeguswa na kilio cha askofu huyu anaweza kumsaidia kwa kupitia M-PESA namba 0758 902 884 au AIR TEL MORNEY 0786 557 612 na Mungu atawabariki wote watakaojitolea kuokoa maisha yake.
No comments:
Post a Comment