Naomba niseme kuwa, sishangai hata kidogo kwa mwanasiasa
kuhama chama hiki na kwenda chama kingine. Hii ni kwasababu mwanasiasa ni kama
mmea, hustawi kwenye mazingira unaopendezwa nayo. Shida yangu ni kwa wale
wanaompokea mwanasiasa huyo na historia yao. Sijui wanaficha wapi nyuso zao
leo. Je, nao wanakenua? Soma maandishi ya raia mmoja hapa chini. Nimeyaweka
kama yalivyo:-
#NAWAHURUMIAAA.
nimeumia lkn naamini kuna watu wameumia zaidi.
#KUBENEA
utaandika nini kakaangu mana uliandikaga lowasa ainunua act kwa mil
200,uliandikaga ZITTO anatumiwa na fisadi lowasa.je Leo utaweza kuandika
aliofika nao bei na utatueleza ni kiasi gani?..uliandika makala kibao
kuthibitisha ufisadi wake na jinsi anavyopenda kununua uongozi.je utaandika
kwamba alipo ndo kapanunua? je utaanza kuungana na fisadi??
#MPENDAZOE.
kaka nimeziona jitihada zako za kukipigania chama kwa
maandiko ktk gazeti la raia mwema.kaka we ndo mwanasiasa pekee ktk historia ya
tanzania uliyehama chama kwa kuchukia mwenendo wake wengine wanaohama wakitoswa
ktk uchaguzi ni wasaka tonge lao.uliandika makala kutufumbua kuhusu huyu lowasa
na wewe jinsi umjuavyo na ukasema ulitoka ccm kuwakimbia watu kama yeye.leo
amekaribishwa kwa heshma we unajiskiaje kaka?? utaendelea kumuita fisadi au
kumnadi??
#MSIGWA.
uliwahi kusema mtanzania atakayemchagua lowasa anatakiwa
akapimwe akili.natamani kujua umeupokeaje ujio wake au umeshapimwa akili.tupe
matokekeo ya vipimo??
#DR.SLAA
pale mwembeyanga ulimtaja lowasa kuwa miongoni mwa watu
hatari ktk nchi yetu,ukamuita fisadi papa na ukasema ushahidi unao kama
anabisha aende mahakamani wewe utakwenda kutoa ushahidi huko.je utatupa huo
ushahidi au nasi tutalindana.hivii nawe utasimama kumnadi!.
#MBOWE.
ulimuita lowasa ni dhaifu na hachukii rushwa bali rafiki wa
rushwa,je kuamua kuungana naye au kumpa nafasi kutatafsirikaje??.wakati
unamnadi utamuita jembe au mdhaifu??
nawafikiria pia rafiki zangu wa kule jamiiforums wakivyokuwa
wakitoa mpaka dokument kuthibitisha ufisadi wake,wakasambaza na video za
nyerere akimzungumzia lowasa na za chama zikimpopoa lowasa.sijui watapokeaje
ujio wake??
INANIUMA SANA
No comments:
Post a Comment