Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Unicef Dkt Jama Gulaid akitoa hotuba katika sherehe ya makabidhiano ya magari ya kubebea wagonjwa Mkoa wa Mbeya15 Octobar 2015 |
Mwakilishi UNICEF Dkt Jama Gulaid kulia akimkabidhi Kaimu katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Ndugu Kastro Msigala taarifa muhimu za magari hayo yenye thamani ya shilingi mil 700 . |
Timu ya Uendeshaji wa huduma za za Afya Mkoa wa Mbeya |
Meza kuu katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Mbeya na wawakilishi wa Shirika la UNICEF. |
Meza kuu katika picha ya pamoja na waganga wakuu wa Halmashauri za Mkoa wa mbeya . |
Meza Kuu katika picha ya Pamoja na timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya Mkoa wa Mbeya . |
Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi shirika la UNICEF. |
SHIRIKA la
Umoja wa Mataifa linalo shughulikia
watoto Duniani (UNICEF) limekabidhi msaada wa magari kumi ya Kubebea wagonjwa yenye tahamni ya shilingi
mil 700.7 kwa serikali ya Mkoa wa Mbeya .
Aidha
shirika hilo lina mpango wa kuboresha vituo 184 vya kutolea huduma za afya
katika mkoa huo wa mbeya ambavyo ni vituo afya na hospital 30 pamoja na
zahanati 154 sanjali na kuvipatia vifaa
muhimu vya kutolea mafunzo kwa watumishi wake.
Akizungumza
katika hafla hiyo iliyofanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Octobar 15
mwaka huu Mwakilishi wa shirika la UNICEF
nchini Tanzania Dkt Jama Gulaid amesema
shirika hilo limetenga kiasi cha shilingi bilioni 2 kwa ajili ya mradi huo.
Amesema
mchango wa UNICEF katika sekta afya na lishe hapa mkoani mbeya imepanua wigo
kutoka halmashauri mbili za mkoa huo hadi kufikia halmashauri zote katika
kipindi cha miaka miwili .
Aidha Dtk,
Jama amesema katika kukabiliana na magonjwa na vifo vya watoto na wanawake
wajawazito ,UNICEF imechangia vifaa tiba muhimu ikiwa ni pamoja vile vya uchunguzi
wa ujauzito ,upasuaji sanjali na vifaa
kuwasaidia watoto wachanga kupumua mara wanapo zaliwa na vifaa vingine vya
utoaji wa huduma katika idara ya uangalizi maalumu ICU.
Aidha amewataka viongozi hao wa mkoa wa Mbeya
kuhakikisha wanaweka juhudi kubwa zaidi katika kupunguza vifo vya akina mama na
watoto wachanga kwa kuhakikisha kwamaba kina mama wajawazito wote wanapata
huduma za afya bure kwa wakati.
Awali
akisoma taarifa ya huduma za afya ya
uzazi na mtoto katika mkoa mbeya mratibu wa huduma za afya ya uzazi na mtoto
Ndugu Prisca Butuyuyu amesema toka
shirika hilo la UNICEF lianze kufanya
mwaka 2012 huduma za afya zimeimalika kwa kiasi kikubwa hususani kwa kuweza
kuzuia vifo vya uzazi na vya watoto wachanga.
Amesema kwa
ujumla hali ya vifo hususani vilivyokuwa
vinatokea katika vituo vya huduma vimepungua kutoka 140 kwa mwaka 2012 na kufikia vifo 94 kwa kwa
mwaka 2014 pamoja na kupunguza vifo vya watoto wachanga kutoka 602 kwa mwaka
2012 hadi kufikia 568 mwaka 2014 ambapo punguzo
hilo ni sawa na asilimia 33.9 na 5.7 kwa watoto wachanga.
Akipokea
msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Kaimu katibu Tawala Ndugu Kastro
Msigala amelishukuru shirika hilo kwa msaada wa magari hayo sanjali na kutoa
wito kwa viongozi wa halmashauri ambao
ni wakurugenzi na waganga wakuu kuhakikisha wanayatunza magari hayo ili yaweze
kutoa huduma stahiki kwa wananchi.
Msaada huo
wa magari imegawanywa katika halmashauri zote mkoa huo wa mbeya ambazo ni
Ileje,Mbozi,Mbeya vijijini,Rungwe,Busokelo,Mbarali pamoja na Kyela na Momba .
Mwisho
(Imeandaliwa na
Jamiimojablog Kanda ya Nyanda za juu kusini Mbeya 0759406070 )
No comments:
Post a Comment