Kikosi hicho ndicho kikubwa zaidi cha waangalizi wa kimataifa Tanzania
Waangalizi wa muda
mfupi kutoka Muungano wa Ulaya (EU EOM) wamewasili nchini Tanzania kwa
ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumapili.
Waangalizi hao 60
waliwasili jijini Dar es Salaam jana na wanatarajiwa kutumwa katika
maeneo mbalimbali ya nchi hiyo kuanzua Jumanne.
Wataungana na
waangalizi wa muda mrefu wa muungano huo ambao wamekuwa wakifuatilia
maandalizi ya uchaguzi pamoja na kampeni tangu mwisho wa mwezi Septemba.
Waangalizi hao wa muda mfupi wanafikisha 140, jumla ya waangalizi waliotumwa na Muungano wa Ulaya kuangalia uchaguzi huo.
"Tutakuwa na waangalizi 140 watakaotembelea vituo vya kupiga kura kwenye maeneo ya mijini na vijijini, kwenye
Mikoa yote, ili kuangalia upigaji na kuhesabiwa kwa kura,” amesema Mwangalizi Mkuu wa EU, Judith Sargentini.
“Waangalizi wetu watafuatilia pia uorodhoshwaji wa matokeo, ambazo ni sehemu muhimu ya tathmini ya jumla ya
EU EOM ya mchakato wa uchaguzi.”
Waangalizi
hao wa uchaguzi watakuwa nchini Tanzania hadi Novemba 15 na
wanatarajiwa kutoa tathmini ya awali kuhusu uchaguzi huo muda mfupi
baada ya kumalizika kwa uchaguzi wenyewe.
No comments:
Post a Comment