Timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wametwaa
ubingwa wa kombe la Chan baada ya kuichapa Mali kwa mabao 3-0.
Mabao ya washindi ya Congo yalifungwa na Meshak Elia
aliyefunga bao mbili wakati Jonathan Bolingi alifunga goli jingine kukamilisha
ushindi wa DR Congo.
Mwaka 2009 DR Congo ilichukua kombe hilo kwa mara ya kwanza
kwa kuifunga Ghana kwa magoli 2-0 kwenye mchezo wa fainali.
Kwenye mashindano ya mwaka huo Tanzania pia ilishiriki
michuano hiyo lakini ilitolewa kwenye hatua ya makundi.
DR Congo imechukua kitita cha dola za Marekani 750,000
wakati mshindi wa pili ambayo ni timu ya Mali yenyewe ikiondoka na dola za
Marekani 400, 000 huku mshindi wa tatu timu ya taifa ya Ivory Coast
ikijishindia dola 250,000
No comments:
Post a Comment