Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akiongea na Ujumbe kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa(hawapo pichani). Ujumbe huo wa Washiriki wa Mafunzo wametembelea Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza katika ziara yao ya Mafunzo kuhusu Uendeshaji wa shughuli za Magereza hapa nchini.
Wakufunzi wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati yao na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani). Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa, Bregedia Jenerali, Jairos Mwaseba.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo mafupi kwa Washiriki wa Mafunzo kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa walipotembelea Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga kwa ziara yao ya Mafunzo(kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Mwandamizi wa Magereza, Augustine Mboje.
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo kutoka chuo cha Ulinzi wa Taifa wakimwangalia mmoja wa wafungwa ambaye amepatiwa ujuzi gerezani wa kukata vitambaa vya nguo tayari kwa kushona nguo za wafungwa waliopo magerezani kama anavyoonekana katika picha katika Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa, Bregedia Jenerali, Jairos Mwaseba alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam akiwa pamoja na Washiriki wa Mafunzo katika chuo hicho cha Ulinzi wa Taifa(hawapo pichani) leo Februari 5, 2016(kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akisalimiana na Mkufunzi wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa ambaye ni raia kutoka China(katikati) ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa, Bregedia Jenerali, Jairos Mwaseba alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam akiwa pamoja na Washiriki wa Mafunzo katika chuo hicho cha Ulinzi wa Taifa(hawapo pichani) leo Februari 5, 2016.
No comments:
Post a Comment