MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imetangaza
bei elekezi ya mafuta itakayoanza kutumika kuanzia leo, inayoonyesha
kuwa petroli imeshuka kwa Sh38.35 wakati dizeli ikipanda kwa Sh6.95 na
mafuta ya taa kwa Sh9.35.
Wiki mbili zilizopita, bei ya rejareja
ya petroli ilipanda kwa Sh70.12 sawa na asilimia 3.57 wakati dizeli
ilipanda kwa Sh 44.88 sawa na asilimia 2.38 na mafuta ya taa kwa Sh
33.02 sawa na asilimia 1.77.
Katika kipindi hicho, petrol jijini
Dar es Salaam iliuzwa kwa kwa Sh 2,102 kwa lita moja ikilinganishwa na
Sh2,031, wiki nne zilizopita..
Kupanda na kushuka kwa bei ya
nishati hiyo ya mafuta kwa lita, ni sehemu ya utekelezaji wa kanuni ya
ukokotoaji inayotumiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na
Maji (Ewura).
Ukokotoaji huo hufanyika kutokana na kushuka kwa
bei ya nishati hiyo katika soko la dunia na kushuka au kuimarika kwa
thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani.Hata hivyo,
katika ukokotoaji huo, jana Ewura ilisema bei za rejareja kwa
petroli imeshuka na bei ya dizeli na mafuta ya taa, imepanda.
Bei katika baadhi ya miji mikuu
Ilifafanua
kwamba, petroli imeshuka kwa Sh38.35 kwa lita ambayo ni sawa na
asilimia 1.82, huku dizeli ikipanda kwa Sh16.95 kwa lita sawa na
asilimia 0.85 na mafuta ya taa yamepanda kwa Sh 9.35 kwa lita sawa na
asilimia 0.48.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, bei kwa miji mikuu
ikiwamo Dares Salaam, petrolil itauzwa kwa Sh2063, dizeli Sh2,016 na
mafuta ya taa Sh 1,976.
Arusha petroli itauzwa kwa Sh 2,147 dizeli 2, 100 na mafuta ya taa Sh2,060.
Ewura
ilizitaka kampuni za mafuta nchini kanza kufanya mabadiliko ya bei kwa
kubandika bei mpya zinazoanza kutumika leo na kuonya kwamba, kampuni
ambazo hazitafanya hivyo zitachukuliwa hatua za kisheria.
Mamlaka
hiyo pia imewataka watumiaji wa nishati hiyo kuhakikisha kuwa wanapata
stakabadhi ya malipo, ambayo itatumika kama kithibitisho i cha mnunuzi
kama kutakuwa na malalamiko.
Mvutano kupinga kanuniKanuni hiyo ya ukokotoaji iliwahi kuibua mvutano mkubwa baina ya Ewura na kampuni za kuuza mafuta nchini Agosti 2 mwaka huu.
Mvutano
huo ulitokana na uamuzi wa Ewura kutangaza kushusha bei ya mafuta
ambapo petroli ilishuka kwa Sh202.37 kwa lita ambayo ni sawa na
asimilia 9.17, dizeli ilishuka kwa Sh173.49 ambayo ni sawa na asilimia
8.32 na mafuta ya taa yalishuka bei kwa Sh181.37, sawa na asilimia 8.70.
Uamuzi
huo uliibua mvutano kati ya wamiliki wa kampuni za mafuta na serikali
huku wamiliki hao wakitunisha msuli na kugoma kuuza nishati hiyo muhimu.
Lakini,
Agosti 10 serikali ilitoa saa 24 kwa kampuni hizo za mafuta kutangaza
kwanini yasichukuliwe hatua za kisheria kwa kukiuka agizo halali la
serikali.
Ewura baadaye ilitoa onyo kwa kampuni zilizogoma
ikiwemo Engen, Camel Oil, huku ikimfungulia mashtaka Mkurugenzi Mkuu wa
BP, kwa kushindwa kutii amri ya kushusha bei.
Siku 11 baada ya
kushusha bei na nchi kutikiswa na mgomo, Ewura ilipandisha tena bei kwa
kisingizio cha kuporomoka kwa shilingi na kupanda kwa bei ya nishati
hiyo katika soko la dunia.
Hata hivyo, wiki mbili zilizopita hadi kuishia jana Ewura ilitangaza kupandisha bei tena ya mafuta na kutoa.
No comments:
Post a Comment