Wakiongoza
ligi, hawajufungwa, uongozi mzuri wa tofauti ya mabao, so far
Manchester United sio timu ya kuwa na wasiwasi na performance yao msimu
huu.
Defence
yao inaweza kuchukua sifa katika uongozi huu wa timu yao, wameruhusu
mabao matano tu kwenye mechi 7, ni rekodi ya kuvutia, tena ukizingatia
matatizo ya majeruhi kwenye safu ya ulinzi tena kipindi hiki ambacho
viraka kama John O’shea na Wes Brown wakiwa wameondoka kwenda
Sunderland.
Pamoja
na rekodi nzuri kwenye safu ya ulinzi, United msimu huu ndio timu
iliyopigiwa mashuti mengi kuliko timu yoyote kwenye ligi, wakipigia
mashuti 97 langoni mwao katika michezo 7.
TAKWIMU
Kwenye
graph hapo juu takwimu zinaonyesha United wame-concede shots 13 au
zaidi katika kila mchezo.Mchezo dhidi ya Stoke City ndio mchezo pekee
ambao United hawakuruhusu shots nyingi.
Pia
kwenye graph nyingine hapo chini inaonyesha katika michezo saba, United
wameruhusu mashuti mengi langoni mwao kuliko waliyopiga.
MAHALI YALIPOPIGWA MASHUTI
KWANINI?
Turudi
kwenye swali-kwanini? Kupitia ushahidi wa takwimu unaonyeshwa hapo juu,
kwanini United wameruhusu kupigiwa mashuti kutoka kwenye umbali mrefu?
Haya ni baadhi ya mambo yanayoweza kuwa majibu kwanini United
wamepigiwa sana mashuti mengi langoni mwao.
1: FIKRA ZA DAVID DE GEA KUWA NA UDHAIFU KWA MIPIRA YA MBALI?
Baada
ya kufungwa bao la mbali na Edin Dzeko katika mechi ya ngao ya hisani,
watu wengi walianza kuhoji udhaifu wa De Gea katika kuzuia mipira ya
mbali.Kupitia
system ya Opta takwimu zinaonyesha De Gea alikuwa na rekodi mbovu
katika kuzuia mashuti ya mbali msimu uliopita katika La Liga.
Je
ni kweli De Gea ni mdhaifu kwa mipira ya mbali? Katika kesi hii sio
rahisi kupata jibu sahihi ukizingatia kipindi kifupi alichocheza,
lakini la kuzingatiwa ni kwamba wapinzani wanafikiri De Gea ana udhaifu
huo, na ndio maana wamekuwa wakijaribu kumtungua kutokea umbali wa 20+
yards.Hitimisho ni kwamba Da Gea bado hajafungwa goli nje ya box katika
premier league.
2: MAJERUHI KWENYE ULINZI
Rio
Ferdinand na Nemanja Vidic wote wamekuwa majeruhi, Chris Smalling na
baadae Antonio Valencia wamekuwa wakichezeshwa katika nafasi beki wa
kulia.United defence wame-cope vizuri na hali hii ya majeruhi, lakini
swali ni kwamba je wameweza kujenga partnership nzuri kwenye ukuta wao,
particularly wakati beki wa kati mmoja anapoenda mbele mwingine anakuja
na ku-cover, kama goli la Fernando Torres @Old Trafford
lilivyoonesha.Ferdinand na Vidic wamekuwa na wakitengeneza partnership
nzuri ya namna hiyo tofauti na Phil Jones na Evans.
3: HAKUNA KIUNGO MZURI MZUIAJI
Kuna
utata whether Micheal Carrick ni kiungo mzuiaji au sio, lakini ni mzuri
zaidi ya wote wawili Anderson na Tom Claverley katika uzuiaji, Ferguson
amekuwa akipenda midfield partnership katika msimu huu.Mtindo wa
kuvutia wa 4-4-2 wa United msimu uliopita ndio ulikuwa chanzo cha
mchezo mzuri wa United msimu uliopita kupitia viungo Micheal Carrick,
Paul Scholes, Fletcher, na Anderson ambao Ferguson alipenda kuwatumia
kama two passer na two runners kwa pamoja.
Cleverley
ni kiungo mzuri sana, akicheza zaidi kwa mtindo wa kushambulia zaidi
kuliko kiungo yeyote aliyetajwa hapo juu, na kumtumia yeye na Anderson
kunaacha gap kubwa katika midfield na defence.Carrick, akiwa yupo mbali
na kuwa mtu mzuri kufanya tackling, lakini bado kuna wengine
wanm-favour yeye kucheza katika nafasi, yupo vizuri katika kufanya
tracking and intercepting.United wanaweza kuwa bora bila yeye, lakini
katika uzuiaji sio wagumu kabisa.
4: ROONEY HAFANYI KAZI KUBWA?
Kama
Stewart Robson alivyosema hivi karibuni, Rooney akiwa katika form nzuri
kama true namba 10 amekuwa akimbii sana bila kuwa na mpira.Alikuwa
anafanya kazi kubwa kipindi wakati akicheza pembeni kipindi United
ilipokuwa dominated na Cristiano Ronaldo na alifanya kazi kubwa zaidi
alipokuwa anatumika kama mshambuliaji pekee.Sasa, mfano mzuri wa aina
yake ya mchezo kuwa madhara ilikuwa katika fainali ya Champions league
dhidi ya Barca, matatizo ya safu ya kiungo cha United yalianzia kutokana na aina hii mchezo, Rooney akiwa hashuki sana kuja kukaba na ku-cover, matokeo yake viungo walikuwa wakifanya kazi kubwa mbele kwenye pitch, na wakiacha gap kubwa nyuma yao.
Sababu nyinginezo.
Performance
ya katika kombe la ngao ya hisani ilionyesha utofauti mkubwa kutoka kwa
United ya msimu uliopita.In 2010/11walikuwa well defined na organized
vizuri.Sasa, wanacheza zaidi wakiwa katika mtindo wa free-flowing and
flexible, matokeo yake wanakuwa wanashambulia zaidi kwa pamoja katika
ushirikiano mzuri lakini wakiachia nafasi zaidi kwa wapinzani katika
midfield.Katika mtindo wa uchezaji wa sasa wachezaji kama Ashley Young
na Nani watakuwa favoured kuliko Ji sung Park na Antonio Valencia
wachezaji ambao ni wazuri katika kucheza kwa nidhamu kubwa ya ukabaji.
HITIMISHO
Sifa
ya De Gea ya kuwa mbovu kwa mipira ya mbali inaonekana wazi kuchangia,
na kama Rooney ataendelea kucheza mchezo wa kutokushuka chini, then
Cleverley na Anderson watakuja kuwa exposed na timu yoyote nzuri kubwa
kama Real Madrid au Barca katika stages za mbele msimu huu.
Tatizo la majeruhi kwa United halionekani kuchangia sana , Evans, Jones na Smalling wanaonekana kucheza vizuri sana.
KWA HISANI YA SHAFFIH BLOG
No comments:
Post a Comment