MABINGWA wa England, Manchester
City jioni hii wametumia vizuri mwanya wa kadi nyekundu aliyopewa Branislav
Ivanovic kwa kutwaa Ngao ya Jamii, wakitoka nyuma kwa bao 1-0 na kuifunga Chelsea
mabao 3-2.
Fernando Torres alifunga
bao la kuongoza dakika ya 40 na dakika ya 42, Chelsea wakabaki 10 baada ya
Ivanovic kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Aleksandar Kolarov.
Mabao ya kipindi cha
pili dakika ya 53 lililofungwa na Yaya Toure, Carlos Tevez dakika ya 59 na
Samir Nasri dakika ya 65 yalitosha kuwapa Man City Ngao na kuuanza msimu vema.
Ryan Bertrand aliifungia
Chelsea bao la pili dakika ya 80.
Off the mark: Manchester City captain Vincent Kompany lifts the Community Shield
We'll drink to that: Nigel De Jong (left) and Carlos Tevez party on the pitch at Villa Park
RAHA YA MECHI USHINDI: Samir Nasri akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao la tatu
UJUMBE KIFUANI: Carlos Tevez akionyesha ujumbe wa maandishi kwenye fulana yake ya ndani ya jezi
BAO LA TATU: Nasri akishangilia bao la tatu alilofunga
BAO LA PILI KIULAINI: Tevez akifunga la pili
KADI NYEKUNDU: Ivanovic akitolewa nje na refaKevin Friend
BAO LA KWANZA: Torres akimtungua Pantilimon
Torres na Kompany
PICHA KWA HISANI YA DAILYMAIL.CO.UK
No comments:
Post a Comment