Diamond Platinumz alikuwa mshiriki kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za MTV MAMA mwaka huu na kwa bahati mbaya hakushinda tuzo katika vipengele vyote viwili. Alivyokuwa akiwania.
Msanii
mkongwe Profesa Jay ambaye anakumbukwa kwa kufanya mapinduzi kwenye
muziki na kuwashawishi wazazi kuwaruhusu watoto wao kuimba kupitia kazi
zake, amemuandikia ujumbe Diamond kupitia Instagram.
“Hapo ulipofika tayari wewe ni Mshindi mkubwa na Unayeipeperusha juu
sana Bendera yetu ya TANZANIA, Wote tunaoitakia mema nchi yetu tuko
nyuma yako Mpaka kieleweke, Usife moyo Kwani hii ni dalili njema ya
kupata mafanikio zaidi na zaidi, Stay blessed and LET’S GO GET THEM!!!”
No comments:
Post a Comment