Maelfu ya walimu nchini Kenya wameanza mgomo wakidai maslahi zaidi, ambao umeathiri shule nyingi za msingi nchini humo.
Walimu hao wamedharau amri ya mahakama ambayo ilibatilisha mgomo huo kwamba sio halali.
Shule nyingi zilizotembelewa na waandishi wa BBC Nairobi na Mombasa zilikuwa zimefungwa.
Walimu wanataka mshahara uongezwe kwa asilimia 100 na 300%.
Walimu
wa shule za sekondari na wale wa vyuo vikuu wamesema watajiunga katika
mgomo huo baadae wiki hii, wakati vyuo vyao vitakapofunguliwa kwa muhula
mpya.
Hadi sasa serikali bado haijazungumza lolote kuhusu mgomo huo.
Mhariri a amesema mgomo huo unaonekana kushika kasi.
Katika
jiji la Nairobi waalimu wamebeba mabango baadhi yao limeandikwa "
Waalimu hatuwezi kula panya na tumechoka na ahadi zisizotekelezeka.
Mgomo huo wa waaalimu umeitishwa na chama cha waalimu unaowawakilisha 250,000.
No comments:
Post a Comment