ISRAEL imeshambulia
maeneo ya wapiganaji katika ukanda wa Gaza kwa siku ya tano (Novemba
18, 2012), wakishambulia kwa ndege na jeshi la majini wakati jeshi lake
lingine likijitayarisha kufanya mashambulizi ya ardhini. Misri hata
hivyo inaona ishara za uwezekano wa kupatikana usitishaji wa mapigano
hapo katika siku za baadaye.
Wapalestina
47, karibu nusu yao wakiwa ni raia, ikiwa ni pamoja na watoto 12,
wameuwawa katika mashambulio hayo ya Israel , maafisa wa Palestina
wamesema. Karibu maroketi 500 yaliyofyatuliwa kutoka Gaza yamefika
nchini Israel, na kuuwa watu watatu na kuwajeruhi wengine kadha.
Israel
ilianzisha mashambulizi yake makubwa ya anga siku ya Jumatano, na kumuua
kiongozi mkuu wa tawi la kijeshi la Hamas, kwa lengo la kuwazuwia
wapiganaji katika eneo hilo la pwani kushambulia kwa maroketi jamii
inayoishi katika eneo lake la kusini mwa nchi hiyo.
Taifa
hilo la Kiyahudi limeshambulia hadi sasa kwa makombora 950 kwa kutumia
ndege za kijeshi dhidi ya eneo hilo dogo la pwani la Wapalestina,
wakilenga vifaa vya kijeshi pamoja na kubomoa nyumba za wapiganaji na
makao makuu.
Mashambulio
yaliendelea usiku wa manane Jumapili, huku ndege za kivita
zikishambulia maeneo kutoka baharini. Shambulio la anga lililenga katika
jengo mjini Gaza ambalo ni la ofisi za chombo cha habari cha Kiarabu na
kuwajeruhi waandishi watatu wa televisheni ya al Quds, kituo cha
televisheni ambacho Israel inakiona kuwa kinaunga mkono kundi la Hamas,
wamesema watu walioshuhudia.
Mashambulio
mengine ya alfajiri dhidi ya nyumba katika kambi ya wakimbizi ya
Jebalya yamesababisha kifo cha mtoto mmoja na kuwajeruhi watu wengine
12, wamesema maafisa wa hospitali. Mashambulio haya yanafuatia taarifa
za kikaidi zilizotolewa na msemaji wa kijeshi wa Hamas Abu Ubaida,
ambaye amesema katika mkutano na waandishi habari kuwa, “duru hii ya
mapambano haitakuwa ya mwisho dhidi ya maadui wa kizayuni na ndio kwanza
inaanza.”
Shambulio la Israel siku ya Jumamosi limeharibu nyumba ya kamanda wa Hamas karibu na mpaka na Misri.
Israel hata hivyo ikiwa na vifaru na vifaa vingine vya kijeshi imeweka majeshi yake katika mpaka, ikiashiria kuwa bado inafikiria uwezekano wa mashambulio ya ardhini ndani ya Gaza. Baraza la mawaziri la Israel limeamua siku ya Ijumaa, (16.11.2012) kuongeza mara dufu idadi ya wanajeshi wa akiba katika operesheni ya Gaza kufikia 75,000 na wanajeshi wa akiba wanaofikia 16,000 tayari wamekwishaitwa.
Israel hata hivyo ikiwa na vifaru na vifaa vingine vya kijeshi imeweka majeshi yake katika mpaka, ikiashiria kuwa bado inafikiria uwezekano wa mashambulio ya ardhini ndani ya Gaza. Baraza la mawaziri la Israel limeamua siku ya Ijumaa, (16.11.2012) kuongeza mara dufu idadi ya wanajeshi wa akiba katika operesheni ya Gaza kufikia 75,000 na wanajeshi wa akiba wanaofikia 16,000 tayari wamekwishaitwa.
Israel
imesema kuwa shule katika eneo lake la kusini zitafugwa leo
Jumapili(19.11.2012) kuepuka madhara zaidi kutokana na mashambulio ya
maroketi ambayo yamefika hadi katika mji mkuu Tel Aviv katika siku
chache zilizopita.
Ndege za
Israel zilishambulia Makao Makuu ya Hamas huko Gaza ikiwemo ofisi ya
waziri mkuu baada ya baraza la mawaziri la Israel kuidhinisha kuandaliwa
kwa wanajeshi wa akiba 75,000 kwa uwezekano wa kuvamia Gaza.
Ndege
hizo za Israel zimeshambulia wizara ya ulinzi na jengo la ofisi ya
Waziri Mkuu Ismail Haniyeh ambapo hapo Ijumaa alikutana na Waziri Mkuu
wa Misri. Kwa siku kadhaa miripuko mizito imekuwa ikilitingisha eneo la
Gaza linalokaliwa na idadi kubwa ya watu na kusababisha kufuka kwa moshi
mzito angani.
No comments:
Post a Comment