Sehemu ya
vijana wakiwa katika picha tatu tofauti mara baada ya kuchoma moto na
kufunga barabara barabara kuu ya Dodoma-Morogoro kwa kuweka vizuwizi
mbalimbali hali iliyopelekea watumia wa barabara hiyo kushindwa kuitumia
kwa masaa matano kabla ya polisi kutuliza hali hiyo iliyoanza majira ya
saa 2 asubuhi na kudumu hadi majira ya saa 7 mchana katika mji mdogo wa
Dumila wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.
Vijana
wakazi wa Dumila na vitongo vyake wakiangusha gari aina ya Land Cruizer T
241 AMS mali ya mfugaji katika barabara kuu ya Dodoma-Morogoro wakati
wa vurugu zilizodumu kwa masaa sita kwa kuweka vizuwizi kwa lengo la
kumshinikiza mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bebdera kusikiliza kero za
wakulima.
Askari wa kutuliza ghasia (FFU) Morogoro wakiangalia gari mara baada ya kuharibiwa wakati wa vurugu hizo kabla ya kulinyanyua.
Gari
hili likionekana mara baada ya kuharibiwa likiwa katikati ya barabara
kabla ya kusukumwa na kulirejesha sehemu ambayo iliegeshwa.
Mwananchi
akizngumza jambo na askari wa kuliza ghasia muda mfupi kabla ya mkuu wa
mkoa wa Morogoro Joel Bendera kuhutubia wananchi hao na amani kurejea
katika hali yake ya kawaida.
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Morogoro (RCO),
Hamisi Selemani kushoto akiawaangalia vijana waliokuwa wakiimba nyimbo
mbalimbali wakati wakimsubiri mkuu wa mkoa wa Morogoro ili awahutubie.
Rasta Man kushoto akijaribu kuwatuliza wananchi wenzake kabla ya mkuu wa mkoa wa Morogoro kuhutubia.
Sehemu
ya akinamama wakionyesha kukerwa na jambo wakati wa vurugu hizo, hapa
walukuwa wakimsubiri mkuu wa mkoa wa Morogoro ili kuweza kusikiliza kero
zao.
Mmoja wa vijana akiwa na kreti ya soda mara baada ya kupora katika vurugu hizo.
Mkuu wa
mkoa wa Morogoro Joel Bendera akiwahutubia umati wa wananchi wa vijijini
vyenye migogoro ya ardhi katika tarafa ya Magole wilaya ya Kilosakwenye
uwanja wa shule ya msingi Dumila jana.
Gari la
mkoa wa Morogoro likiondoa eneo la mkutano wa hadhara uliofanyika
katika eneo la shule ya msingi Dumila wilaya ya Kilosa mkoani hapa.
No comments:
Post a Comment