Baadhi ya
waumini wa Kiislamu Msikiti wa Mtambani wakiwa wamemzunguka askari
Polisi, Jonathan Tossi (katikati aliyeshika kamera) wakimuhoji baada ya
kumshikilia kwa muda, hata hivyo walimuachia kwa masharti ya kumtaka
afute picha zote alizopiga eneo hilo.
Askari Polisi wakizunguka doria eneo la Msikiti wa Mtambani jijini Dar es Salaam kuhakikisha kuna amani.
Askari wa Jeshi la Polisi, Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU)
wakizunguka kufanya doria maeneo mbalimbali ya jijini la Dar es Salaam
kuhakikisha kuna amani. (Picha kwa hisani ya Gazeti la Jambo Leo.)
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BAADHI ya waumini wa Kiislamu Msikiti wa Mtambani Jijini Dar es
Salaam jana wamemkamata mmoja wa askari wa Jeshi la Polisi na
kumshikilia kwa muda kabla ya kumwachia kwa masharti kadhaa. Kwa mujibu
wa chanzo cha habari hizi kimebainisha askari aliyekamatwa ni Jonathan
Tossi ambaye anafanya kazi kitengo cha habari na uhusiano wa Jeshi la
Polisi.
Askari huyo alijikuta akiingia kwenye mikono ya waumini hao alipokuwa
akitekeleza majukumu yake (kazini) akipiga picha mtaani maeneo ya
Msikiti wa Mtambani jijini Dar es Salaam. Taarifa zaidi zinasema baada
ya waumini hao kumkamata askari huyo walimuhoji kwa muda kisha kutaka
kitambulisho chake na kumuamuru afute picha zote alizokuwa akipiga eneo
hilo ili wamuachilie kwa usalama wake.
“Kutokana na kuhofia usalama wake alikubaliana nao na kisha kufta
picha zote alizopiga. Walimtaka pia aoneshe kitambulisho na kuhoji ni
kwanini anapiga picha wakati yeye ni askari…baada ya kukubaliana na
masharti hayo walimuachia,” kilisema chanzo chetu.
“Sisi wenyewe tunashangaa wapiga picha walikuwa wengi wa vyombo
mbalimbali vya habari hatujui hawa walijuaje kwamba yule jamaa alikuwa
askari na wakati alikuwa amevaa kiraia,” alisema shuhuda mmoja aliyekuwa
eneo la tukio.
Leo mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ulinzi na doria
iliim*rishwa na Jeshi la Polisi ambapo magari na pikipiki za Polisi
zikiwa na askari waliojiandaa kutuliza ghasia yalikuwa yakizunguka ikiwa
ni kujiandaa kwa kukabiliana na vurugu zozote.
Mitaa kadhaa mwandishi wa mtandao huu alishuhudia askari walio na
mabomu ya machozi, huku wakiwa wamevalia vifaa maalumu vya kujikinga na
risasi wakizunguka kwenye magari yao maeneo mbalimbali likiwemo eneo la
Msikiti wa Mtambani Kinondoni jijini Da rs Salaam. Hata hivyo hakuna
taarifa za kutokea vurugu zozote.HABARI KWA HISANI YA AUDIFACEJACKSON BLOG
Taarifa ambazo hazikuthibitishwa zinasema doria ya polisi ililazimika
kufanywa baada za kuwepo na taarifa kuwa huenda wafuasi wa Shekhe Issa
Ponda wangelifanya fujo kutokana na kutoridhishwa na hatua ya kukamatwa
kwa kiongozi huyo kwa tuhuma kadhaa zinazomkabili.
Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, kuzungumzia
kwa kina taarifa hizi hazikuzaa matuna. Hata hivyo Thehabari inaendelea
kumtafuta kwa ufafanuzi zaidi wa tukio la kukamatwa kwa askari wao na
kuachiwa.
No comments:
Post a Comment