Waziri
wa uchukuzi Mh. Dkt.Harrison Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari
leo ofisini kwake jijini Dares salaam juu ya hatua zilizochukuliwa na
wizara ya uchukuzi juu ya sakata la madawa ya kulevya yaliyokamatwa
huko afrika kusini hivi karibuni.
Mwakyembe
amewafukuza kazi mtandao mzima uliohusika kusaidia kusafirisha madawa
hayo, pia ameliagiza jeshi la polisi kuwakamata wafanyakazi hao na
kuwaunganisha na wenzao kujibu mashitaka ya jinai.
Waziri wa uchukuzi akionyesha picha ya msanii Agness Gelard maarufu kwa jina la Masogange mbele ya waandishi wa habari. Masogange alikamatwa na madawa ya kulevya huko afrika kusini.
Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Waziri wa uchukuzi
Waziri wa uchukuzi akionyesha picha ya msanii Agness Gelard maarufu kwa jina la Masogange mbele ya waandishi wa habari. Masogange alikamatwa na madawa ya kulevya huko afrika kusini.
Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Waziri wa uchukuzi
PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE DAR ES SALAAM
Na Philemon Solomon wa fullshangwe Dar es salaam
Sakata
la kusafirisha madawa ya kulevya kwenda Afrika kusini limechukua sura
mpya baada ya Waziri mwenye dhamana ya uchukuzi hapa nchini Mh. Dkt.
Harrison Mwakyembe kuchukua hatua kali dhidi yao ikiwamo kuwafukuza kazi
mtandao mzima uliohusika kusaidia kwa namna moja ama nyingine
upitishwaji wa madawa hayo.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake, Waziri Mwakyembe amebainisha
baadhi ya ushahidi uliotumika kugundua mtandao mzima uliohusika kusaidia
kusafirisha mzigo huo wa madawa ya kulevya katika uwanja wa ndege wa
Mwalimu Julius kuwa ni kamera zilizofungwa katika uwanja huo
Dkt.
Mwakyembe aliwataja waliohusika kusafirisha mzigo huo, kuwa ni pamoja
na askari wa polisi, CPl Ernest ambaye alionekana akiwa bize na kuonesha
kila dalili ya kusaidia kusafirisha mzigo siku hiyo
Wengine
ni walinzi wa uwanja huo ambao ni Yusuph Isa, Jackson Manyoni, Juliana
Thadei na Mohamedi Kalungwana ambao wote kwa pamoja walisaidia
kusafirisha madawa hayo na hivyo Waziri kumuamuru muajiri wa wafanyakazi
hao kuwafukuza kazi mara moja na wasikanyage uwanja wa ndege
Pia
askari ambaye amehusika na kula njama za kusafirisha madawa hayo Waziri
amelitaka jeshi la polisi kumshughulikia askari huyo ipasavyo na
kwamba wizara inatarajia askari huyo hawezi kukanyaga tena uwanja wa
ndege
No comments:
Post a Comment