Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimwagilia maji mti wa kumbukumbu aliupanda muda mfupi baada ya kuzindua barabara ya Songea hadi Namtumbo yenye urefu wa kilomita 71.4 katika hafla iliyofanyika katika kijiji cha Migelegele wilayani Namtumbo leo. Wapili kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli, Watatu ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.Servacius Likwelile, Wanne ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Changamoto za Milenia Tanzania Bwana Bernard Mchomvu,Wapili kulia ni mbunge wa Namtumbo Vita Kawawa na kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Mfuko wa Changamoto za Milenia Bwana Karl Fickenscher.
|
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,Balozi Mdogo wa Japan Bwana Kazuyoshi Matsunaga(katikati) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(African Development Bank) ADB Bibi Tonia Kondiero kulia wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuzindua rasmi ujenzi wa Barabara ya Lami ya Namtumbo- Matemanga yenye urefu wa kilomita 128.9 uliofanyika katika kijiji cha Migelegele .Wapili kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli na watatu kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.Barabara hiyo inajengwa na serikali ya Tanzania ikisaidiwa na fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika na serikali ya Japan kupitia shirika lake la misaada la JICA.
|
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mbunge wa Namtumbo Vita Kawawa wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi wakati wa hafla ya uzinduzi wa hospitali mpya ya wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma uliofanyika jana.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bwana Saidi Mwambungu.
Dkt.Jakaya Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Changamoto za millennia(Millenium Challenge Corporation Bwana Karl Fickensher wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi Kuzindua Barabara ya Lami ya Songea-Namtumbo yenye urefu wa kilometa 71.4 iliyojengwa kwa msaada wa Watu wa Marekani kupitia mfuko huo wakati wa hafla iliyofanyika katika kijiji cha Migelegele wilayani Namtumbo leo.
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Changamoto za millennia(Millenium Challenge Corporation Bwana Karl Fickensher wakati wa uzinduzi wa Barabara ya lami ya Songea-Namtumbo yenye urefu wa kilometa 71.4 iliyojengwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na msaada kutoka kwa watu wa Marekani kupitia mfuko huo katika sherhe zilizofanyika katika kijiji cha Migelegele wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma leo. Picha na Freddy Maro
No comments:
Post a Comment