Kiongozi wa
mashtaka nchini Argentina Alberto Nisman amepatikana amefariki nyumbani kwake
baada ya kumshtumu rais wa taifa hilo
Kiongozi
maarufu wa mashtaka nchini Argentine amepatikana amefariki ndani ya nyumba yake
mjini Buenos Aires, baada ya kumshutumu Rais Cristina Fernandez kwa kuzuia
uchunguzi wa mashambulio mabaya zaidi ya ugaidi kuwahi kufanyika nchini humo.
Alberto
Nisman alikuwa amepangiwa kutoa maelezo ya kina kwa bunge la taifa hilo.
Alikuwa
akisimamia uchunguzi kuhusiana na mlipuko katika kituo kimoja cha kijamii
kilichokuwa kikisimamiwa na
wayahudi mjini Buenos miaka 20 iliyopita ambapo
watu watano waliuwawa.
Juma
lililopita bwana Nisman alimshutumu Rais Fernandez na wakuu wengine kwa kuzuia
uchunguzi huo.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment