Waziri wa nishati na madini Mhe. Sospeter Muhongo |
WAZIRI wa nishati na madini Mhe. Sospeter Muhongo amejikuta
katika wakati mgumu na msafara wake baada ya kuzomewa na wananchi wa soko la
wakulima katikati ya mji wa Kahama wakati akitokea kwenye ziara yake vijijini
wilayani Kahama mkoani Shinyanga
Tukio hilo limetokea hivi karibuni wakati waziri huyo na
msafara wake wakitokea kata ya Bulungwa kwenye jimbo la Kahama kuelekea kata ya
Bulige jimbo la Msalala kukagua ujenzi wa mradi wa umeme vijijini unaotekelezwa
na wakala wa umeme vijini nchini (REA) unaoendelea kufungwa katika maeneo
mbalimbali wilayani humo.
Baada ya kufika katika eneo hilo wananchi hao
walianza
kumzomea wakidai ni “mwizi wa fedha zilikuwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow
kelele ambazo ziliwashtua watu wengi ambao walijitokeza kuona anayezomewa ni
waziri yupi.
Hata hivyo kelele hizo ziliisha baada ya msafara wa waziri
huyo ambaye yuko ziara kanda ya ziwa kutokomea na kuacha makundi mbalimbali
katika eneo hilo la soko la wakulima wakijadili hatima yake katika mpango mzima
wa mgogolo wa uchotwaji wa mabililioni ya shilingi kwenye akaunti hiyo ya
Escrow.
Pamoja na kuzomewa na wananchi hao Muhongo katika ziara yake
wilayani Kahama ameacha neema kwa wananchi wa halmashauri ya Ushetu baada ya
kuwaahidi umeme katika awamu ya tatu ya mradi ya nishati vijijini.
No comments:
Post a Comment