Mwanamume mmoja amekiri kumchinja na kisha kumkatakata mkewe
katika nyumba yao mjini London.
Naveed Ahmed, mwenye umri wa miaka 41, alikiri makosa yake
ya kumuua mkewe ambaye ni mama wa watoto wake wawili, Tahira Ahmed, 38.
Mwili wa Bi Ahmed ulipatikana na polisi tarehe 27 mwezi Mei
baada ya majirani kuripoti kwamba walisikia wawili hao wakigombana.
Uchunguzi wa kifo chja mwanamke huyo ilisema kuwa
alipatikana akiwa amekatwa mikono , kudungwa kisu na kisha kukatwakatwa.
Tahira Ahmed alipatikana akiwa amechinjwa nyumbani kwao
mjini London
Bwana Ahmed anatarajiwa kuhukumiwa tarehe 28 mwezi huu
katika mahakama aya Old Bailey.
Inaarfiwa jaji amemuonya kwamba huenda akafungwa jela kwa
mauaji hayo.
Awali Ahmed alikana mauaji ya mkewe wakati kesi ilipoanza
kusikilizwa mwezi Oktoba.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment