Wanasayansi wanasema kwamba wanaweza kueleza kasi ya
mwanariadha maarufu sana duniani Usain Bolt inatokana na nini kwa kutumia
hisabati au hesabu.
Bolt alivunja rekodi kwa kumaliza mbio za mita 100 kwa
sekunde 9.58 wakati wa mashindano ya kimataifa mwaka 2009 mjini Berlin. Na hio
ndio rekodi ya dunia.
Wanasayansi hao wanasema utafiti wao unafafanua kwamba nguvu
na uwezo wa kimwili wa Bolt kustahimili upepo inatokana na urefu wake wa futi 6
inchi 5.
Hata hivyo wanasayansi hao wanasema bado wanafanya uchunguzi
kujua kinachowafanya wanariadha wazuri kama Bolt kukimbia kwa kasi.
Kulingana na utafiti wa wanasayansi hao waliotumia
hesabu,kasi ya Bolt ya sekunde 9.58 mjini Berlin iliwezekana baada ya
mwanariadha huyo kukimbia mita 12.2 kwa sekunde sawa na kasi ya mita 27 kwa
saa.
Walisema kuwa mwili wa Boltulipata kasi yake pindi alipoanza
kukimbia chini ya sekunde moja na hiyo ilikuwa nusu tu ya kasi yake yote.
Bolt baada ya kushinda mbio za dunia
Wanafizikia hao wanasema hii ina maanisha kuwa hapo ndipo
hewa hupunguza nguvu zake za kusongesha vitu.
Pia waligungua kwamba chini ya asilimia nane ya nguvu za
misuli yake ilitumika wakati alipoanza kukimbia.
Rekodi ya Bolt mjini Berlin, ilikuwa nzuri zaidi kushuhudiwa
tangu kuanza kutumika kwa kifaa cha elektroniki kunakili muda wa wanariadha
kukimbia mwaka 1968.
''Ni vigumu sana kuvunja rekodi siku hizi, hata kwa sekunde
moja kwani wanariadha wanahitajika kutumia nguvu nyingi sana dhidi ya upepo
ambao huongezeka kwa kila ongezeko la kasi, '' walisema wanafizikia walofanya
utafiti huo.
John Barrow wa chuo kiuu cha Cambridge alisema kwamba kasi
ya Bolt pia ilitokana na urefu wa hatua zake za miguu licha ya kuanza mbio kwa
kuchelewa kila wakati kipenga kilipopigwa.
"misuli yake inamsaidia sana kuongeza kasi licha ya
kwamba mwenyewe ana kasi.''
Wanasema kwamba Bolt ana uwezo mkubwa wa kuvunja rekodi
zaidi ikiwa ataanza mbio zake bila ya kuchelewa.
No comments:
Post a Comment