Waziri kuu, Kassim Majaliwa akiteta jambo na Askofu Mkuu wa Pili wa EAGT, Dkt. Brown Abel Mwakipesile katika Ibada ya kumsimika Askofu huyo iliyofanyika kwenye kanisa la EAGT Mlimwa West Mjini Dodoma Februari 7, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Ibada ya kumsimika Askofu Mkuu wa Pili wa EAGT, Dkt. Brown Abel Mwakipesile iliyofanyika kwenye Kanisa la EAGT Mlimwa West mjini Dodoma Februari 7, 2016.
Waumini wa EAGT wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika Ibada ya kumsimika Askofu Mkuu wa Pili wa EAGT, Dkt Brown Abel Mwakilpesile kwenye kanisa la EAGT Mlimwa West mjini Dodoma Feb 7, 2016.
Waumini wa EAGT wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika Ibada ya kumsimika Askofu Mkuu wa Pili wa EAGT, Dkt Brown Abel Mwakilpesile kwenye kanisa la EAGT Mlimwa West mjini Dodoma Feb 7, 2016.
Viongozi na waumini wa EAGT wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika Ibada ya kumsimika Askofu Mkuu wa Pili wa EAGT, Dkt Brown Abel Mwakilpesile kwenye kanisa la EAGT Mlimwa West mjini Dodoma Feb 7, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya picha Askofu Mkuu wa Pili wa EAGT, Dkt. Brown Abel Mwakipesilie zawadi ya picha yenye maadishi ya neon la Mungu katika Ibada ya kumsimika Askofu huyo iliyofanyika kwenye kanisa la EAGT Mlimwa West mjini Dodoma Februari 7, 2016. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema ataitisha kikao cha viongozi wa dini zote
hivi karibuni ili wapange na kuainisha ni mambo gani ambayo wanaweza
kutoa ushauri kwa Serikali na kupata njia bora ya kuwahudumia
Watanzania.
Ametoa
ahadi hiyo leo mchana (Jumapili, Februari 7, 2016) wakati akizungumza
na mamia ya waumini walioshiriki ibada ya kumsimika Askofu Mkuu wa Pili
wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Askofu Dk.
Brown Abel Mwakipesile iliyofanyika kwenye kanisa la EAGT la Mlimwa West
nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Waziri
Mkuu Majaliwa ambaye alihudhuria ibada hiyo kwa niaba ya Rais Dk. John
Pombe Magufuli alisema: “Hivi karibuni nitaitisha kikao cha viongozi wa
dini zote kitakachojumuisha Maaskofu Wakuu, Masheikh na baadhi ya
wachungaji ili tukae na kubaini ni nini kifanyike ili kuisadia Serikali
namna nzuri ya kuboresha maisha ya Watanzania.”
Akijibu
risala iliyosomwa na Katibu Mkuu wa kanisa hilo, Dk. Leonard Mwizarubi,
Waziri Mkuu alisema Serikali imeanza kufanya mapitio ambayo
yatawawezesha Watanzania kupata huduma kwa urahisi.
“Katibu
Mkuu pamoja na Baba Askofu Mkuu wamegusia suala la upandaji wa gharama
za vifaa vya ujenzi pamoja na suala la makazi bora. Mwezi ujao tunaanza
vikao vya Bunge vya kupitia bajeti ya Serikali, tutaliangalia hili kwa
kumshirikisha Waziri wa Fedha… tutafanya mapitio katika hili ili
mwananchi wa kawaida aweze kumudu maisha,” alisema huku akishangiliwa na
waumini hao.
Aliwaomba
viongozi wa kanisa hilo pamoja na waumini wake waendelee kuiombea nchi
pamoja na viongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano kwani kazi ya kutumbua
majipu waliyoianzisha ina mitihani mikubwa.
“Kutokana
na maombi yenu kwa viongozi wakuu wa kitaifa nina imani Taifa hili
litafika tunakotaka liende. Endeleeni kutuombea kwa sababu kazi ya
kutumbua majipu ina mitihani mikubwa. Lakini pia napenda niwahakikishie
kuwa Serikali hii itatumbua majipu hayo kwa kufuata sheria, kanuni na
taratibu zilizowekwa. Hakuna mtu ambaye ataonewa,” alisisitiza Waziri
Mkuu.
Kuhusu
mgogoro wa kiwanja cha kanisa hilo kilichopo eneo la Ipagala, Waziri
Mkuu aliahidi kulishughulikia suala lao kesho asubuhi kabla hajaondoka
kurejea Dar es Salaam. “Kesho asubuhi nitamuita Mkurugenzi Mkuu wa CDA
na kumtaka anipe taarifa sahihi kuhusu mgogoro huu. Najua suala hili
liko mahakamani, lakini naamini Mkurugenzi anaweza kuwa kiungo kizuri
kati ya wananchi waliojenga eneo hili pamoja na kanisa ambao mnamiliki
kiwanja husika”.
“Kama
atapata eneo jingine na kupima viwanja, kisha akawapatia hawa wananchi
anaweza kuwa amesaidia kuondoa mgogoro huu. Wananchi walienda mahakamani
huku wakijua eneo lenu limewekewa uzio, sasa wanagoma kutoka kwa sababu
hawana mahali pa kwenda,” aliongeza.
Mapema,
akitoa hotuba yake, Askofu Mkuu Dk. Mwakipesile alisema kanisa
litaendelea kuiombea Serikali ya awamu ya tano ili nchi idumu katika
amani na utulivu.
Aligusia
eneo la kanisa lililopo kiwanja na 34, kitalu ‘E’, Ipagala East,
Dodoma, ambalo ujenzi wa shule yake umesimama kutokana na mgogoro baina
yao na wananchi waliovamia eneo lao kwa kujenga nyumba za kuishi licha
ya kuwa eneo hilo lilikwishawekewa uzio.
“Kama
kanisa tumeshindwa kukamilisha ujenzi wa shule kwa sababu wananchi hao
walifungua kesi mahakamani kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa. Tunaomba
uamuzi wa kesi hii uharakishwe,” alisema huku akishangiliwa.
Alisema
kanisa hilo lina majengo 4,670 nchini kote na viwanja 420 ambavyo ni
vya kujenga makanisa na vituo vya kutoa huduma mbalimbali za kijamii.
Kwa
upande wake, Katibu Mkuu wa kanisa hilo, Dk. Mwizarubi alisema katika
risala yake kwamba wanaiomba Serikali ifikirie kushusha bei ya vifaa vya
ujenzi ili wananchi waweze kuwa na nyumba bora za kuishi.
“Maisha
bora maana yake ni kuwa na nyumba bora. Tunaiomba Serikali yako
ipunguze bei ya vifaa vya ujenzi ili Watanzania waweze kuwa na makazi
bora,” alisema huku akishangiliwa.
No comments:
Post a Comment