Mwenyekiti
wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimshukuru balozi wa
Uturuki Nchini, Dkt Sander Gurbuz, baada ya kupokea msaada wa mashine
10 za kusaidia watoto waliozaliwa kabla ya muda wao. Mashine hizo,
zenye thamani ya dola 30,000 (kama milioni 50), zimetolewa na kampuni ya
madini na nishati ya Uturki iitwayo TPM ambapo Mkurugenzi Mkuu wake Bw
Burak Buyuksaar (wa tatu kulia) alikuwepo kushuhudisa makabidhiano
hayo. Kulia ni mke wa balozi, Mama Durhan Gurbuz. Picha na Ikulu
Ubalozi
wa Uturuki nchini Tanzania umetoa msaada wa incubators 10 zenye
thamani ya Tsh. Mil 50/- kwa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) inayoongozwa na Mhe. Mama Salma Kikwete, Mke wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.
Akikabidhi
msaada huo Balozi wa Uturuki hapa nchini Mhe. Dr. Sander Gurbuz
amesema kuwa wametoa msaada huo kwa ajili ya kusaidia moja ya programu
za Taasisi ya WAMA inayolenga kuboresha huduma za afya ya mama na
mtoto. Pamoja na kudumisha uhusiano mzuri ambao nchi yake ya Uturuki na Tanzania umekuwa nao.
Mhe. Balozi aliambatana na Mke Wake Mama Durhan Gurbuz na Mkurugenzi Mkuu wa TPM Mining and Energy Co. Limited, Bw. Burak Buyuksarac.
Akitoa shukrani baada ya kupokea msaada huo Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mhe. Mama Salma Kikwete amesema kuwa msaada huo ni mkubwa sana na
utasaidia kuokoa maisha ya watoto wachanga ambao wangeweza kufa
kutokana na ukosefu wa vifaa hivi hasa maeneo ya vijijini. Mama Salma
aliongeza kuwa pamoja mazingira ya Vijijini yanaweza yasiruhusu sana utumiaji wa vifaa hivi lakini kwa sababu siku hizi kuna umeme wa jua utasaidia matumizi ya vifaa hivi.
No comments:
Post a Comment