Mechi
namba 78 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Simba iliyochezwa
Oktoba 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh.
337,537,000.
Watazamaji
waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo walikuwa 53,366 ambapo
kiingilio kilikuwa sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000 na sh.
20,000 kwa VIP A.
Baada
ya kuondoa gharama za mchezo na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)
ambayo ni sh. 51,488,694 na gharama za awali za mchezo sh. 27,405,250
kila timu ilipata sh. 77,592,916.
Mgawo
mwingine ulikwenda kwa uwanja (sh. 25,864,305), TFF (sh. 25,864,305),
Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu- FDF (sh. 12,932,152), gharama za
mchezo (sh. 25,864,305), Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es
Salaam- DRFA (sh. 10,345,722) na Baraza la Michezo la Taifa- BMT (sh.
2,586,430).
No comments:
Post a Comment