Hatimaye
aliyekuwa Kocha Mkuu wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Sam Timbe,
ametimka jana jijini Dar es Salaam kuelekea nchini Uganda, baada ya
kulipwa stahiki zake alizokuwa akiudai uongozi wa klabu hiyo baada
kusitisha naye mkataba wa kuinoa timu hiyo.
Ofisa
Habari wa Yanga, Louis Sendeu, alisema jana kuwa tayari wameshamlipa
stahiki zake Timbe ambaye alisitishiwa ghafla mkataba na uongozi wa
klabu hiyo hivi karibuni na kumrejesha kocha wake wa zamani Mserbia
Kostadin Papic.
“Tumeshamalizana
na Timbe kwa kumlipa kilicho chake na ameondoka jana kwenda kwao tayari
kwa masuala yake binafsi,” alisema Sendeu.
Kabla
ya kuondoka, juzi Timbe alikaririwa kwenye vyombo vya habari akiapa
kutoondoka mpaka atakapolipwa fedha zake baada ya kuona akizungushwa
kulipwa malipo yake ambayo ni mishahara ya miezi saba na fidia ya
kuvunja naye mkataba, ambao ulikuwa unatarajiwa kumalizika Mei mwakani.
Hata
hivyo, Sendeu hakuwa tayari kuweka wazi kiasi alicholipwa kocha huyo
kwa madai kuwa ni siri baina ya uongozi na kocha huyo mwenye rekodi ya
mafanikio ya kufundisha soka katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Chanzo
cha habari cha kuaminika kutoka ndani ya uongozi wa mabingwa hao wa TZ
Bara na afrika mashariki na kati kimesema kuwa, Timbe amelipwa shilingi
milioni 36 ambazo zimejumuisha mishahara yake na fidia ya kuvunjiwa
mkataba wake.
No comments:
Post a Comment