Jerry Muro akiongea na waandishi wa habari leo baada ya kuachiwa huru na mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.
Jerry Muro na mke wake wakitoka mahakamani.
Mmoja
kati ya watuhumiwa waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya kuomba rushwa ya
shilingi milioni kumi, Edmund Kapama akitoka katika chumba cha Mahakama
huku akina na furaha kwa kuwa huru.
Nipo huru sasa.
Pascal Kamara wakili wa Jerry Muro akiongea na waandishi wa habari nje ya mahakama ya kisutu.
Pokea Mvinyo Baba.
Waandishi wa habari wakiwa Mahakamani hapo
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imewaachia huru kwa mashitaka
yote matatu yaliyokuwa yakiwakabili aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC) Jarry Muro na wenzake wawili.
Hakimu
Frank Moshi, alisema anawaachia washitakiwa hao kwasababu upande wa
mashitaka umeshindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao pasi shaka.
Muro,
Edmond Kapama pamoja na deogratius Mgasa walikuwa wakikabiliwa na kesi
ya kuomba na kutaka kupokea rushwa ya Sh milioni 10 toka kwa aliyekuwa
Muhasibu wa Wilaya ya Bagamoyo Michael Wage.
Mashitaka
yao yalikuwa ni ya kula njama, kuomba rushwa na kujitambulisha maafisa
wa TAKUKURU shitaka linalowakabili Mgasa na kapama.
Muro
baada ya kutoka mahakamani alitangaza kwa wanahabari kuwasamehe wabaya
wake wote ambao ni viongozi wa serikali baadhi na baadhi ya maafisa wa
polisi na kuwataka waandishi wa habari kushikamana kuendelea kuibua uozo
unaoendelea bila woga.
Katika hukumu, hakimu Moshi alisema baada
ya kuangalia ushahidi mahakama ilikuwa na maswali ya kujiuliza kama
upande wa jamuhuri uliweza kuthibitisha mashitaka dhidi ya washitakiwa
ambapo shitaka la kula njama kwa nia ya kuomba rushwa ambalo linawahusu
washitakiwa wote, ushahidi ulikuwa wa Wage.
Shahidi
huyo wa tatu wa jamuhuri lisema alikutana na Muro kwenye mgahawa wa
Califonia ambapo mawasiliano kati yao yaliendelea kwa njia ya simu ya
mkononi.
Ushahidi
huo ulikuwa hafifu kwasababu upande wa mashitaka haukuweza kuwasilisha
karatasi ya mawasiliano kati yao kutoka kwenye kampuni ya mtandao wa
simu (printout).
Vile
vile alisema picha za CCTV iliyowasilishwa mahakamani ilikuwa ni kivuli
kisichoonyesha sura za watu badala yake wangeleta CD kuonyesha kwenye
video ili watu waweze kutambulika kwa urahisi.
Mawasiliano
ni jambo la msingi kwasababu ili kula njama ni lazima mawasiliano
yafanyike hivyo kuna mapungufu makubwa katika shitaka hilo.
Dereva
aliyemwendesha wa Wage alidaiwa kuwa na Wage pale mgahawa wa Califonia
walipokutana na Muro, alitakiwa kuletwa athibitishe kama Wage na Muro
walikutana upande wa mashitaka hawakumwita shahidi huyo.
Katika
shitaka la kuomba rushwa lilowakabili wote katika ushahidi wake Wage,
alieleza Muro na wenzake walimtaka awapatie Sh milioni 10 watamsaidia
kwenye tuhuma zinazomkabili lakini hakuwa nazo akawapa sh milioni moja
mbali na ushahidi huo hakuna ushahidi mwingine wa serikali unaoonyesha
kuwa walipokea fedha hiyo.
“Mahakama ilitegemea kuwe na ushahidi wa mawasiliano kama haupo wa kuona lakini hayo yote hayakufanyika,” alisema hakimu Moshi.
Muro
alikamatwa ndani ya gari, mahakama haielewi ni kwanini kulikuwa na
haraka hiyo kwanini asingeachwa wakakutana na Wage. Kwa upande wa hotel
ya Sea Cliff ni sehemu ya watu yoyote anaweza kwenda.
Washitakiwa
Mgasa na Kapama hakimu Moshi alisema hawakukamatwa eneo la tukio
walikamatwa na kuunganishwa na halikufanyika gwaride la kuwatambua na
cheti kuletwa mahakamani.
Shitaka
la linalowakabili Mgasa na Kapama la kujitambulisha maafisa wa TAKUKURU
mahakama ilisema halikuthibitishwa lina mashaka. Alisema washitakiwa
walijitambulisha kwa moja anaitwa Dr na mwingine Musa.
Upande wa mashitaka ulitakiwa kufatilia mtaani kama majina hayo washitakiwa walikuwa wakiyatumia lakini hilo halikufanyika.
“Wage
kama msomi ngazi ya uhasibu aliwezaje kukubali mtu ajitambulishe kwa
mdomo kama afisa wa TAKUKURU bila kuonyeshwa vitambulisho na akakubali
mahakama inapata mashaka”.
Aliongeza hakimu huyo hakuna vielelezo na ushahidi wa kuthibitisha bila kuacha shaka hivyo wanaachiwa huru kwa mashitaka yote.
Alisema
Moshi risiti, pingu na miwani havikuwa na mgogoro katika kesi na
kwavile vilipatikana kwa risiti basi arudishiwe muhusika na upande
unataka kukata rufaa wana ruhusiwa. Wakili kiongozi wa kesi hiyo
Boniface Stanslaus alisema taafifa atampelekea Mkurugenzi wa Mashitaka
nchini (DPP) ataamua kama watakata rufaa.
Washitakiwa walifikishwa mahakamani Februari 5 mwaka jana kwa mara ya kwanza mbele ya Hakimu mkazi, Gabriel Mirumbe.
No comments:
Post a Comment