Geoffrey Mutai wa Kenya ameshinda mbio za New York Marathon na kuweka rekodi mpya ya mbio hizo.
Mutai amemaliza katika muda usio rasmi wa saa mbili, dakika tano na sekunde sita,- zaidi ya dakika mbili ya muda wa zamani.
Mkimbiaji huyo mwenye umri wa miaka
30, sasa amejiweka katika wakimbiaji ambao wanadhaniwa watan'gara katika
michuano ya Olimpiki ya mwakani, baada ya kuweka rekodi ya pili mwaka
huu.
Mwezi Aprili, Mutai alikimbia kwa kasi ya kihistoria katika mbio za Boston: 2:03:02.
Hata hivyo muda huo haukutajwa kama rekodi ya
dunia kwa sababu njia ya mbio hizo inadhaniwa kuwa imenyooka sana na ina
mteremko mkali.
muda wa wakimbiaji katika nafasi ya pili na ya
tatu ulikuwa ndani ya rekodi ya zamani ya mbio za New York ya 2:07:43
iliyowekwa na Tesfaye Jifar wa Ethiopia miaka kumi iliyopita.
Bingwa wa mbio za marathon za London Emmanuel
Mutai wa Kenya, alimaliza dakika moja na sekunde 22 nyuma ya Geoffrey
Mutai. Tsegaye Kabede wa Ethiopia alimaliza katika nafasi ya tatu.
Geoffrey Mutai na Emmanuel Mutai hawana uhusiano wowote wa kindugu.
Mfumo wa Manka kuimarisha huduma za kifedha katika utoaji wa mikopo
-
*Mfumo ni kwa ajili ya kuchakata taarifa za fedha.
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
Tausi Africa imezindua rasmi Manka ambao ni mfumo wa uchambuzi wa kifedha...
5 hours ago
No comments:
Post a Comment