Newcastle imendeleza rekodi yake
ya kutopoteza mchezo tangu msimu msimu huu wa ligi ulipoanza wakati
Ryan Taylor bao lake la pili lilipoizamisha kabisa Everton.

Hekaheka katika lango la Everton
Lakini kikosi cha Alan Pardew kilisimama imara na kujihakikishia kubakia nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi.
Newcastle kwa sasa haijapoteza mchezo katika ligi tangu walipopoteza mchezo kwa kufungwa mabao 3-0 mwezi wa Mei dhidi ya Liverpool msimu uliopita, lakini wanakabiliwa na mtihani mgumu katika mechi zao tatu zijazo.
Robin van Persie akiwa amefunga bao la kwanza na kutengeneza mengine mawili, aliisaidia Arsenal kushinda mfululizo michezo minne iliyopita ya ligi kuu ya England. Arsenal iliizamisha West Bromwich Albion mabao 3-0.

Robin van Persie
Arsenal iliendelea kumiliki kipindi cha pili na Vermaelen, Gervinho na Aaron Ramsey nusura wangefunga mabao.
Bao la tatu la Arsenal lilipachikwa na Mikel Arteta.
Manchester United imeendeleza furaha ya miaka 25 ya umeneja wa Sir Alex Ferguson katika klabu hiyo, baada ya kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Sunderland.

Wes Brown alijifunga mwenyewe dhdi ya Man United
Manchester United walibadilika kipindi cha pili na kucheza vizuri lakini hawakuweza kuongeza bao jingine.
Javier Hernandez alipiga kichwa mpira uliokuwa ukielekea wavuni lakini ukaokolewa katika mstari wa lango na Wayne Rooney pamoja na Patrice Evra walijaribu mikwaju lakini iliokolewa.
Akiwa amefunga bao lake la sita la msimu huu wa ligi Frank Lampard alifanikiwa kuipatia ushindi finyu Chelsea wa bao moja kwa bila dhidi ya Blackburn inayokabiliwa na mzozo wa mashabiki kumkataa meneja.
Lampard alifunga bao hilo kwa kichwa baada ya kupokea pasi ya pembeni ya Branislav Ivanovic.

Mfungaji wa bao pekee la Chelsea Frank Lampard
Na chagizo zikiendelea kupamba moto dhidi ya Kean, Yakubu na Grant Hanley walikosa nafasi nzuri za kufunga na pia mlinzi Gael Givet mkwaju wake ukagonga mwamba.
Mabao mawili aliyofunga Darren Bent na jingine la Gabriel Agbonlahor yameisaidia Aston Villa kuzoa pointi tatu dhidi ya Norwich.

Darren Bent akishangilia bao
Agbonlahor baadae akatumia makosa ya Leon Barnett kurudisha pasi nyuma na kuipatia Villa bao la pili kabla ya kumtengenezea nafasi ya kupachika bao la tatu Bent.
Steve Morison aliipatia Norwich bao la pili kwa kichwa.
Nayo Liverpool ikicheza katika uwanja wao wa Anfield ilibanwa na Swansea City na kwenda sare ya kutofungana.
Mlinda mlango wa Swansea Micel Vorm alifanya kazi ya ziada kuwanyima wenyeji bao dakika za mwisho baada ya kuokoa mkwaju wa beki Glen Johnson aliouchia kutoka yadi 20, lakini Andy Caroll mwanzoni mwa mchezo alipoteza nafasi nzuri ya kufunga bao.
No comments:
Post a Comment