Klabu
ya Vancouver Whitecaps ya nchini Canada inayoshiriki Ligi kuu nchini
Marekani imemtoa kiungo wa kimataifa toka Tanzania Nizar Khalfan kwenda
kwenye klabu ya Philadelphia Union ambayo kama Whitecaps inashiriki ligi
ya MLS . Whitecaps imemruhusu Nizar kwenda Philadelphia katika mchakato
wa maalum wa kubadilishana wachezaji wa ligi hiyo maarafu kama Waver
Player Draft.
Nizar Khalfan ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Mtwara,
ameichezea Whitecaps katika michezo 22 ya ligi ya MLS kwa mwaka 2011
ambapo alianza michezo 9. Katika dakika 1,066, kiungo huyu mwenye umri
wa miaka 23 alifunga bao moja huku akitoa pasi 4 za mabao kwa wenzake .
Nizar
alijiunga na Whitecaps katikati ya msimu wa mwaka 2009 wakati klabi
hiyo bado ikiwa kwenye ligi daraja la kwanza na kwa jumla amecheza
michezo 58 ambayo ni sawa na dakika 3,029 .
Khalfan alianza soka lake
nchini Tanzania akiwa na klabu ya Mtibwa Sugar kwenye msimu wa mwaka
2005/06 na katika msimu wa mwaka 2006-7 aliichezea Moro United.
Katika
misimu hiyo miwili Nizar alicheza michezo 57 akifunga mabao 16 akiwa na
Mtibwa na mabao matano katika katika michezo 16 akiwa na Moro United.
Katikati ya misimu hiyo miwili Nizar alicheza soka la kulipwa nchini
Kuwait
Khalfan ameichezea timu ya taifa ya tanzania Taifa Stars katika michezo 25 ya kimataifa na amefunga mabao matano,
Khalfan
alifunga bao la ushindi katika mchezo wa kihistoria dhidi ya Burkina
Faso kwenye uwanja wa taifa wa Dar es salaam tarehe 2 septemba 2006
kwenye uwanja wa taifa Dar es salam, na pia alifunga bao la nne kwenye
ushindi wa 4-1 dhidi ya Mauritius septemba 6 mwaka 2008.
Hivi
karibuni Khalfan aliichezea timu yake ya taifa katika mchezo wa kufuzu
kwa mataifa ya afrika ambapo alitoa pasi ya bao lililofungwa na Mbwana
Samatta kwenye mchezo dhidi ya Algeria ulioisha kwa sare ya 1-1, na pia
alianza kwenye michezo yote miwili ya awali ya kufuzu kwa kombe la dunia
2014 ambako timu yake ilifuzu kuingia kwenye kundi lenye timu za Ivory
Coast, Morocco na Gambia.
KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA CMA KWA UANZISHWAJI WA MFUMO WA KIDIJITALI.
-
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeipongeza Tume
ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kwa uanzishwaji wa Mfumo wa Uendeshaji na
Us...
3 hours ago
No comments:
Post a Comment