Na Mashaka Baltazar,MWANZA
WANANCHI WA Wilaya
ya Sengerema Mkoa wa Mwanza, wameitaka Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Serikali za Mitaa, kufika wilayani humo ili
kujionea uozO na ubadhirifu wa fedha za umma unaofanywa na watendaji wa
Halmashauri ya wilaya hiyo.
Sakata hilo
limeibuka hivi karibuni katika kikao cha Baraza la
Madiwani wa halmashauri hiyo, kufuatia ripoti ya ukaguzi maalumu,
uliofanywa na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Fedha za Serikali
(CAG) Ludovick L. Utoh, baada ya Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Matthew
Lubongeja kuwataka madiwazni wasijadili ripoti hiyo akidai ilikuwa ya
siri.
Madudu hayo ya ubadhirifu wa fedha za umma
yameibua mgawanyiko mkubwa miongoni mwa Madiwani wa Halmashauri ya
Wilaya ya Sengerema, kufuatia ofisi ya CAG, kuanika katika ripoti ya
ukaguzi wake ubadhirifu mkubwa wa fedha za miradi ya maendeleo.
Kutokana
na ubadhirifu huo CAG amependekeza uongozi wa halmashauri hiyo,
uwachukulie hatua za kinidhamu na kuwasimamisha kazi watendaji wake
tisa kwa madai ya kukiuka sheria, taratibu na kanuni za utendaji kazi.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa
watendaji wa halmashauri hiyo hawafuati sheria,taratibu na kanuni
katika utendaji wao kazi kuhusiana na miradi ya maendeleo inayotekelezwa
na halmashauri, ambapo pia ilibaini kuwa fedha shilingi bilioni 1.5
zilitengwa kwa ajili ya idara ya kilimo hazikutumika bila sababu katika
kipindi cha miaka miwili.
Madiwani hao walipinga kutojadiliwa kwa
ripoti hiyo ikiwa ni pamoja na kuukataa ushawishi wa Mkuu wa Wilaya hiyo
Elinansi Pallangyo kutotaka ijadiliw, waaakidai kuwa kikao hicho ndicho
chenye maamuzi ya mwisho
Kwa mujibu wa chanzo chetu madiwani hao
walichachamaa na kutaka ripoti hiyo iletwe na kujadiliwa kisha kuchukua
hatua kulingana na mapendekezo ya CAG, ambapo Mwenyekiti baada ya
kuzidiwa nguvu alimwagiza Mkurugenzi wa halmashauri Eric Mussika
kuileta na ikapitiwa kifungu kwa kifungu.
Madiwani
baada ya kupitia ripoti hiyo walibaini kutokamilika kwa miradi mingi ya
maendeleo, wakati fedha zimetolewa kwa ajili ya miradi ya maji,barabara
na ujenzi wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu, huku miradi
mingine fedha zikiwa zimehamishwa bila idhini ya vikao kutoka akaunti
moja kwenda nyingine.
Katika ripoti hiyo ya ukaguzi huo CAG
(nakala tunayo) ilibaini kuwapo kwa ucheleweshaji wa ujenzi wa majengo
nabaadhi yamejengwa chini ya kiwango hivyo kutolingana kwa thamani ya
fedha zilizolipwa kwa wakandarasi.
Mmmoja wa Madiwani wa
halmashauri hiyo alisema kuwa waqtendaji hao hawafuati sheria za manunui
na hakuna uwazi wan a musada wa kutosha katika utangazaji wa zabuni
mbalimbali , kweamba halmashauri haina daftari la kumbukumbu ya miradi
husika kwa mujibu wa agizo Na.6(e) na 50 ya kanuni ya fedha za Serikali
za Mitaa,ya mwaka 1997.
“Kwa ujumla CAG amebaini ubadhirifu
katika miradi ya ujenzi wa majengo,barabara na maji.Watendaji wa
halmashauri wanakiuka sheria za manunuzi ya umma kwa kutozuingatia
kifungu cha 37 (4) ya sheria ya manunuiz ya umma , kumesababisha uteuzi
wa wajumbe wa timu ya tathmini wasio na ujuzi wa kai yauthamini” alisema
mmoja wa madiwani kwa sharti la kutojwa jina
Alisema ripoti ya mkaguzi huyo wa
hesabu za serikali ilileza kuwa halmashauri hiyo haina mchanganuo wa
kazi unaojumuisha kodi la ongezeko la thamani na inamtaja Mhandisi wa
Maji Elikali Edward kuwa, uzembe wa kutoandaa makisio ya ufanyaji kazi
kabla ya mradi kuanza na ni moja ya mapungufu yanyoisababishia hasara
halmashauri hiyo.
Wengine waliotajwa katika ripoti
hiyo maalumu ni pamoja na Afisa Mipango wa Wilaya hiyo,Kaimu Mweka
hazina,Mwenyekiti wa Bodi ya zabuni, Afisa Ugavi wa Wilaya,Mhandisi wa
Ujenzi, Mwanasheria wa Halmashauri, Meneja wa Mamlaka ya maji safi na
majitaka na Mhasibu wa Mamlaka ya maji safi na majitaka.
Aidha Mwenyekiti wa halmashauri hiyo
Lubongeja alitaka hoja hiyo ya kusimamishwa kwa watendaji hao iahirishwe
hadi Novemba 6 mwaka huu ili Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , Ndikilo aweze
kuhudhuria.
Mmoja wa madiwani wa halmahauri hiyo, Hamis Tabasamu alipinga
hoja hiyo akidai kuwa ni kupoteza fedha za walipa kodi kwa vile kikao
kimoja hugharimu shilingi milioni 16 za kulia posho wajumbe 46 ambapo
kila mmoja hulipwa shilingi 175,000 hali iliyosababisha atolewe nje ya
kikao na mwenyekiti, baada ya kusisitiza watumishi waliotajwa katika
ripoti hiyo ya CAG wasimamishwe kisha mashitaka yao
yafuate kama ilivyobainisha taarifa hiyo ya ukaguzi maalum.
Wananchi wa wilaya hiyo wamedai kuwa kama
watumishi hao hawaatchukuliwa hatua basi
hawana imani na uongozi wa halmashauri hiyo chini mwenyekiti na
mkurugeni wake na kupendekeza kamati ya bunge ya seriali za mitaa
kufanya uchunguzi wa ubadhirifu huo .
Endapo hilo halifanyika basi wananchi hao wako tayari
kuifikisha halmashauri yao mahakamani ikiwa ni pamoja na mwenyekiti kwa
madai kuwa alishiriki kusaini mikataba mibovu isiyo na tija.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya CAG ambayo nakala
yake imepelekwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi (Ikulu), Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
na kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, inawataka makandarasi waliolipwa
bila kufuata taratibu kurejesha fedha hizo halmashauri, wengi wakiwa ni
wale waliopewa zabuni za miradi ya majengo, maji na barabara.
No comments:
Post a Comment