Imeandikwa na Idd Seif
Klabu ya Arsenal ilianzishwa na kundi la
wafanyakazi wa kiwanda kilichokua kikitengeneza silaha kilichojulikana
kama Woolwich Arsenal Armament Factory walipoamua kuunda klabu ya mpira
wa miguu mnamo mwaka 1886. Klabu hiyo ikacheza chini ya jina ''Dial Square''.
Mnamo mwaka 1891 klabu hio ikabadili hadhi yake na kua ya wachezaji wa kulipwa na kubadili jina kua Woolwich Arsenal, na hatimaye kujiunga na Ligi ya soka mnamo mwaka 1893. Mnamo mwaka 1913, klabu hio ikahamia uwanja wa Highbury kaskazini mwa jiji la London ikichezea katika daraja la pili. Baada ya vita vikuu vya kwanza vya Dunia Arsenal ilikubaliwa kwa kura katika Ligi ya daraja la kwanza lililopanuliwa, na tangu hapo hadi leo Arsenal wamesalia katika Ligi kuu.
Kwa bahati mbaya Kocha huyo Chapman alifariki katikati ya msimu wa neema ambapo tayari alikua ameisha jipatia sifa ya stadi wa kufundisha soka.
Mrithi wake akawa George Allison aliyeendeleza mtindo wa kutawala soka kwa muongo mzima, akishinda Kombe la FA mnamo mwaka 1936 na ushindi mwingine mnamo mwaka 1938. Katika kipindi hiki Arsenal ilijivunia baadhi ya wachezaji mahiri, Alex James, Ted Drake, Cliff Bastin, David Jack, Eddie Hapgood na George Male ni majina ya baadhi ya wachezaji wazuri kuwahi kusakata gozi katika Ligi ya soka.
Vita vikuu vya pili vya dunia viliiathiri Arsenal lakini Tom Whittaker alipoteuliwa kua kocha matokeo yakaimarika na ufanisi kupatikana. Arsenal ilishinda Ligi ya mwaka 1947/48 na 1952/53; vilevile ikashinda Kombe la FA la mwaka 1950 na kumaliza wa pili mnamo mwaka 1952. Miaka ya 60 haikua na mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kushindwa kwenye fainali mbili za kombe la FA la mwaka 1968 na 1969 . Wakati huu Arsenal ilikua na kocha mpya, Bertie Mee aliyeiwezesha kushinda Kombe lake lwa kwanza la Ulaya mnamo mwaka 1969/70, ilipoichabanga Anderlecht 4-3 katika mechi mbili za ugenini na nyumbani.
Mambo mazuri yalijitokeza msimu uliofuata. Timu ya Arsenal ikiwa na wachezaji waliokuja jijengea majina kama Charlie George, George Armstrong, Ray Kennedy pamoja na nahodha wa Frank McLintock, walishinda Ligi na Kombe la FA kwa mpigo'. Waliweza kuupata ushindi kwenye uwanja wa mahasimu wao wa White Hart Lane, kisha wakaizaba Liverpool baada ya kipindi cha ziada kushinda Kombe la FA kwenye uwanja Mkuu wa Wembley. Timu hio ilirudi uwanja wa Wembley kwa fainali tatu mfululizo chini ya Kocha Terry Neill mwishoni mwa muongo - kwa ushindi wa 3-2 dhidi ya Manchester United. Mechi hio ilipata uimaarufu kama fainali ya dakika tanol'. The Gunners pia waliweza kufikia fainali ya Kombe la mshindi la mwaka 1980, wakiwa na wachezaji kama Graham Rix, Frank Stapleton, Pat Rice, David O'Leary na Liam Brady, lakini wakapoteza fainali hiyo kupitia mikwaju ya matuta dhidi ya klabu ya Valencia.
George Graham
Mnamo mwaka 1986 George Graham, mmoja wa wachezaji wa Timu ya mwaka 1970 iliyoshinda vikombe viwili vya mwaka 1971 alichaguliwa kuwa meneja kutoka kwa Don Howe naye akaleta mafanikio zaidi. Aliiwezesha Arsenal kushinda Kombe lake la kwanza la Ligi la mwaka 1986/87, kwa kuichapa Liverpool 2-0 kwenye uwanja wao wa Anfield.
Ushindi mwingine ulifuata msimu wa mwaka 1990/91, klabu hio iliposifika kwa mabeki wake wanne, waliopoteza mechi moja msimu mzima.
Mnamo mwaka 1997/98, Arsenal ilimpata mwalimu mpya, Arsene Wenger na katika msimu wake wa kwanza kwenye uwanja wa Highbury, Arsenal ikafanikiwa kwa kuweka rekodi ya kushinda vikombe viwili Ligi na Kombe la FA. Hili lilimuzesha Mfaransa huyu kushinda zawadi ya mwaka ya Carling kama Meneja bora. Dennis Bergkamp pia alitangazwa kua mchezaji bora wa wandishi wa habari pamoja na mchezaji bora wa wachezaji wanaocheza soka ya kulipwa. Ukawa msimu mzuri kwa klabu uliomalizika kwa wachezaji wawili klabu hio Emmanuel Petit na Patrick Vieira kuiwakilisha klabu katika kikosi cha Ufaransa kilichoshinda Kombe la Dunia mwaka 1998.
Msimu wa mwaka 2000 Arsenal ilimaliza ya pili ikishinda medali za fedha ikishiriki fainali ya kombe la Uefa ambapo ilimaliza kwenye fainali ikishindwa katika fainali. Mwaka 2001 klabu hio ikaishia kwenye robo fainali ya michuano ya Ligi ya mabingwa UEFA ilipoondolewa na Valencia.
Msimu wa Mwaka 2001/2002 hata hivyo yakatokea mabadiliko na klabu hio kushinda mataji mawili kwa mpigo ilipoichapa Chelsea katika Kombe la FA na kumaliza Ligi kwa mechi 13 bila kupoteza na ushindi wa kuridhisha wa bao 1-0 dhidi ya mahasimu wao Manchester United kwenye uwanja wa Old Trafford. Hivyo Arsenal ikaendelea msimu mzima bila kupoteza kwenye uwanja wake kwa msimu. Kutokana na hilo Arsene Wenger akatajwa kama Meneja bora wa Barclaycard huku mcheza kiungo Robert Pires akishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa wandishi wa habari.
Msimu uliofuata Arsenal ilikosea kosea kutetea taji lake ingawa Gunners ilijitokeza kua klabu ya kwanza ya England katika zaidi ya kipindi cha miaka 20 kutetea taji lake la FA kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Southampton kwenye uwanja wa Cardiff. Mwaka huo Thierry Henry akashinda tuzo ya wanfdishi wa habari na pia ya wacheza soka ya kulipwa katika mwaka uliomuomuezesha kujiunga na miamba ya wachezaji kama Dennis Bergkamp waliofunga mabao 100.
Msimu wa 2003/2004 Arsenal ikashinda tena Ligi kuu ya soka bila kushindwa msimu mzima ikimaliza pointi 11 mbeke ya Chelsea. Arsenal ilivunja rekodi kadhaa ikielekea ushindi wake wa mara ya 13 wa Ligi ya England. Msimu huo ndipo alipowasili kijana mdogo Cesc Fabregas mwezi January na hadi mwisho wa Msimu akawa ameisha vunja rekodi ya mchezaji mwenye umri mdogo kushiriki mechi nyingi akiwa mwenye umri wa miaka 16 na siku 177.
Msimu wa mwisho kwenye uwanja wa Highbury ulikua wa mwaka 2005/06 na katika sherehe za kuuaga uwanja huo Arsenal ilimaliza Ligi katika nafasi ya nnena Ligi ya mabingwa. Rekodi ya Arsenal kwa hivyo kwenye uwanja wake wa Highbury ukawa mzuri wa kusifika. Ilicheza mechi 2,010, ilishinda mechi 1,196, ikatoka sare 475, na kupoteza mara 339, ikafunga jumla ya mabao 4,038, ikifungwa mabao 1,955.
Muhimu katika safari ya klabu hio kufikia fainali ya Ligi ya mabingwa mjini Paris mwaka 2005/2006. Ni mechi 12 bila kupoteza, ikiwa ni pamoja na kuweka rekodi mpya ya mfululizo wa mechi bila kufungwa bao hata moja(mechi 10). Mafanikio haya yaliiweka klabu hii kwenye barabara ya kuonana uso kwa uso na Barcelona katika fainali ya Ligi ya mabingwa dhidi ya Barcelona mjini Paris kwenye uwanja wa Stade de France.
Uwanja wa Emirates
Mnamo mwezi Julai mwaka 2006 Arsenal ikahama kutoka uwanja wa Highbury, uwanja wake wa miaka 93, na kuhamia kwenye uwanja wake mpya. Klabu ya Ajax ikawa mpinzani katika mechi ya kumuaga mchezaji aliyesifika na kuichezea Arsenal akiweka rekodi hadi nyingine Dennis Bergkamp. Na katika mechi hi ambapo Bergkamp alishiriki mechi yake ya mwisho ikiwa ni mechi ya kwanza kabisa kwenye uwanja mpya wa Emirates.
No comments:
Post a Comment