Rais
Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa chama cha UDP Bw. John
Momose Cheyo katika hafla ya kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania
iliyofanyika usiku huu kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam,
huku mtandao wako wa FULLSHNAGWE ukikuletea matukio haya kutoka viwanja
vya Ikulu moja kwa moja.
Wageni mbalimbali
wakiwemo viongozi wa Serikali, Mawaziri, Wabunge na Mabalozi na waalikwa
mbalimbali wamehudhuria katika hafla hiyo iliyokua na burudani za
vikundi vya ngoma kutoka sehemu mbalimbali.
Rais
Dk. Jakaya Kikwete akifurahia jambo na wageni waalikwa wakati alipokuwa
akipita sehemu mbalimbali na kuwasalimia katika viwanja vya Ikulu huku
akiwatakia sherehe njema ya miaka 50 ya Uhuru.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion na magazeti ya Dira na Hekaheka
Viwanjani Bw. Alex Msama akibadilishana mawazo na Waziri wa Habari,
Vijana , Utamaduni na Michezo Dk Emmanuel Nchimbi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion na magazeti ya Dira na Hekaheka Viwanjani Bw. Alex Msama akisalimiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri mkuu - Sera na Uratibu wa Bunge,Mh. William Lukuvi katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na wageni waalikwa katika hafla hiyo iuliyofanyika viwanja vya Ikulu usiku huu
Wakuu
wa taasisi mbalimbali za Serikali walikuwepo kutoka kulia ni Clement
Mshana Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Helman Hokororo, Mkuu wa vikosi
vya Zimamoto ACF Fikiri S. Salla, mdau Esther Baruti na mpiga picha wa
Idara ya habari Maelezo John Lukuwi wakijadili jambo.
Mdau
John Melele Mkuu wa Utawala CCM makao makuu Ofini ndogo Lumumba akiwa
na Nancy Mukoyogo kulia na Upendo Mazzuki nao wamehudhuria katika hafla
hiyo ya miaka 50 ya uhuru.
Makamu
wa Rais Dk. Gharib Bilal akisalimiana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa
Mataifa nchini Alberic Kacou katika viwanja vya ikulu wakati wa hafla ya
miaka 50 ya uhuru wa Tanzania iliyofanyika usiku huu jijini Dar es
salaam.
No comments:
Post a Comment