:Afisa
Habari wa UN Information Centre (UNIC) Usia Nkhoma Ledama
akiwakaribisha wageni waalikwa katika semina ya mafunzo kwa vijana juu
ya matumizi ya mtandao katika kuhamasisha haki za Binadamu iliyofanyika
katika Ofisi za UN Information Centre.
Afisa
Habari wa United Nation Information Centre Bi. Stella Vuzo akisoma
ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kuhusiana na
Azimio la Umoja wa Mataifa lililopitishwa mwaka 1948 lenye vipengele 30
ambavyo vimeainisha Haki Msingi za Binadamu na Uhuru.
Mtaalamu
wa IT na Mwanaharakati wa Haki za Binadamu kutoka Kamisheni ya Haki
za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) Bw.Wilfred Warioba akielezea jinsi
mitandao ya Kisasa ya Mawasiliano kama vile Facebook, Twitter na Blogs
zinavyofanyakazi na zinavyoweza kutumika kupashana Habari na
Kuelimishana ambapo pia amesema iwapo itatumika vibaya inaweza kuelta
madhara makubwa kwa watumiaji. Katikati ni Mzungumzaji Mkuu Mwalikwa
kutoka CHRAGG Bw. Ayoub Rioba na Afisa Habari wa United Nation
Information Centre Bi. Stella Vuzo.
Baadhi ya wanafunzi kutoka Shule za Chang'ombe, Ruvu Sekondari, IST, Kibasila, Loyola na TEYODEN wakifuatilia mafunzo hayo.
Mwanafunzi wa Kidato cha Tano Janeth Absalom kutoka Loyola High School akichangia mada wakati wa mafunzo hayo.
Afisa
Habari wa Temeke Youth Development Network (TEYODEN) Humphrey Shao
akifafanua jambo kuhusiana na matumiz ya mitandao kama njia ya
mawasiliano.
Wanafunzi
wakiwa wameshika Poster yenye Ujumbe maalum unaonyesha kwamba Binadamu
wote ni sawa bila kujali aina ya Ulemavu mtu alionao.
Mgeni
rasmi katika mafunzo hayo Vicky Ntetema kutoka Taasisi inayotetea haki
za jamii ya watu wenye Ulemavu wa Ngozi ya Under the Same Sun akieleza
jinsi watu wengine wanavyoweza kutumia mitandao hiyo kukiuka haki za
msingi za Binadamu kwa namna mbalimbali na kuwataka vijana kuwa makini
na kuepuka kupeana ahadi za kukutana na watu wasiowajua waliowasiliana
nao kupitia mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter na Blogs.
No comments:
Post a Comment