Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, November 28, 2011

MALAWI YAINYUKA HARAMBEE STARS 2-0 UWANJA WA TAIFA


Steve Chagoma kulia wa timu ya Malawi akivaana na Paul Were wa Harambee Stars katika mchezo wa kombe la TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011 uliofanyika leo jioni kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam huku timu ya Malawi ikiibuka na magoli 2-0 dhidi ya Harambee Stars ya Kenya. (PICHA NA MOHAMED MAMBO-DAR ES SALAAM)
Bob Mugalia wa Harambee Stars akimruka mlinda mlango wa timu ya Malawi Charles Swini katika mchezo wa mashindano ya Kombe la TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011 uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa leo jioni.
wachezaji wa malawi na Kenya wakipambana vikali kwenye goli la malawi katika mchezo huo uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam

MILOVAN ASAINI MKATABA WA MIEZI SITA KUIFUNDISHA SIMBA..

KOCHA MPYA WA SIMBA MILOVAN CIRKOVIC AKISAINI MKATABA KWENYE HOTEL YA MOVEN PICK JIJINI DAR ES SALAAM.

HAPA AKIWA NA MWENYEKITI WA SIMBA ALHAJ ISMAIL ADEN RAGE.


MWENYEKITI WA KAMATI YA UFUNDI IBRAHIM MASOUD 'MAESTRO ' ALIKUA SHUHUDA WA TUKIO HILO.KWA HISANI YA SHAFFIH BLOG


EXCLUSIVE: KOCHA MPYA WA SIMBA MILOVAN CIRKOVIC ALIPOWASILI BONGO JANA

Baada ya kuwasili nchini, kocha Mserbia Milovan Cirkovic akilakiwa na katibu mkuu wa klabu ya Simba Evodius Mtawala kulia, na mwenyekiti wa kamati ya Ufundi ya klabu hiyo Ibrahim Masoud "Maestro" na wa mwisho kushoto ni Jerry Yambi mjumbe wa kamati ya mashindano ya klabu hiyo.

Kocha Mserbia Milovan Cirkovic aliyewasili nchini jana usiku kwa mazungumzo ya kuinoa timu yake ya zamani Simba sports club mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Dar es salaam, ambapo alipokewa na mwenyekiti wa kamati ya ufundi ya klabu hiyo Ibrahim Masoud "Maestro" kulia, wengine ni daktari msaidizi Shindika na Kit Manager Kessy.


Milovan baada ya kuwasili nchini akijiandaa kuondoka uwanjani hapo sambamba na mwenyekiti wa kamati ya ufundi Maestro na daktari msaidizi wa timu hiyo Shindika, kulia ni kit manager Kessy

"Karibu tena Simba" Milovan na mwenyekiti wa kamati ya ufundi ya klabu ya Simba Maestro.

UKATILI DHIDI YA VIKONGWE KWA IMANI ZA KISHRIKINA ULIOKUWA UMESHAMIRI MIKOA YA KASKAZINI SASA VYASHAMIRI MKOANI MBEYA


Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60(Pichani), akiwa hoi jana siku ya jumapili baada ya kupingwa na wananchi wenye hasira kali Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya wakimtuhumu kujihusisha na inami za kishirikina.
Mkuu wa kituo cha polisi cha Iyunga(kushoto) na Mwenyekiti wa kitongoji cha Ikuti Bwana Emanuel Mwasote(katikati mwenye shati ya pink) wakijaribu kuokoa maisha ya Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60(Pichani), kwa kumpeleka Kituo cha polisi Iyunga, baada ya wananchi wenye hasira kali kuvamia kwenye nyumba yake na kutaka kuichoma moto jana siku ya jumapili kabla ya kupingwa na wananchi wenye hasira kali Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya wakimtuhumu kujihusisha na inami za kishirikina. Hata hivyo juhudi hizo ziligonga mwamba baada ya wananchi hao kuwazidi nguvu polisi kutokana na  Jeshi la polisi kushindwa kufika mapema eneo la tukio na kuaanza kumdondoshea kichapo.
 Bwana Richard Mwakalinga akijaribu kuokoa maisha ya Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60(Pichani),wakati wananchi wa kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga jijini hapa kuanza kumdondoshea kichapo jana siku ya jumapiliwakimtuhumu kujihusisha na inami za kishirikina, wakati Jeshi la polisi halijafika eneo la tukio ili kuwedha kuwadhibiti wananchi hao.
Wananchi wenye hasira kali Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya, wakimpiga kwa mawe Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60(Pichani), hapo jana siku ya jumapili  wakimtuhumu kujihusisha na inami za kishirikina.
 Hapa ni nyumba ya Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60, kabla ya kuvunjwa na yeye akiwa ndani ya nyumba hiyo baada ya kutuhumiwa na wananchi wa kitongoji alichokuwa akiishi Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya kujihusisha na imani za kishirikina.
 Wananchi wenye hasira kali wakivunja nyumba ya Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60, jana siku ya jumapili, baada ya kutuhumiwa na wananchi wa kitongoji alichokuwa akiishi Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya kujihusisha na Imani za kishirikina.
 Wananchi wa kitongoji alichokuwa akiishi Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya wakimzingira Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60, kabla ya kumdondoshea kichapo wakimtuhumu kujihusisha na imani za kishirikina.
Wananchi wenye hasira kali wakiendelea kuvunja nyumba ya Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60, jana siku ya jumapili, ambapo akina mama nao hawakukaa nyumba kushiriki tukio hili, baada ya kutuhumiwa na wananchi wa kitongoji alichokuwa akiishi Kitongoji cha Ikuti kata ya Iyunga, jijini Mbeya kujihusisha na Imani za kishirikina.
 Baada ya kupingwa  Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60, jana siku ya jumapili, Jeshi la polisi lilifanikiwa kufika eneo la tukio  na kumchukua mzee huyo na kumpeleka Hospitali ya Rufaa iliyopo jijini Mbeya. Pichani ni baadhi ya askali na raia wema wakimuchukua mzee huyo na kumpeleka kwenye gari la polisi kabla ya kumkimbiza hospitali.
 Mke wa Mzee Asumwisye Mwakambinda mwenye umri wa miaka 60, katikati akilia kwa uchungu na kupewa msaada na wanawake wenzake, baada ya mumewe  kudondoshewa kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali Kitongoji cha Ikuti, kata ya Iyunga jijini Mbeya jana siku ya jumapili wakimtuhumu kujihusisha na imani za kishirikina.(Picha na habari na Ezekiel Kamanga)

HITIMISHO
Maoni ya mtandao Jeshi la polisi linapaswa kufika kwa wakati muafaka mara baada ya kupewa taarifa, lakini pia elimu itolewe kwa wananchi kutojichukulia sheria mikononi kwani tuhuma na sio uthibitisho, kwani mahakama pekee ndio ina mamlaka ya kutoa hukumu.