Na Mwandishi Wetu
MPIGA
ngoma nguli wa bendi ya muziki wa dansi ya African Stars 'Twanga
Pepeta', James Kibosho, amerithi mikoba ya aliyekuwa mwimbaji wa bendi
hiyo, Charles Gabriel 'Chaz Baba' aliyetangaza kujiengua wiki hii na
kuhamia Mashujaa Musica.
Mmoja
wa wanamuziki galacha wa Twanga Pepeta, Khamis Kayumbu 'Amigolas' jana
usiku wakati wa onesho la Twanga Pepeta kwenye ukumbi wa Club
Bilicanas, alimtangaza Kibosho kuwa ndiye kiongozi wa kupanga muziki
jukwaani (Stage Master), nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Chaz Baba.
Tangazo
hilo la Amigolas lilipokewa kwa hoi hoi, nderemo na vifijo kutoka kwa
mashabiki kochokocho wa Twanga Pepeta waliojaa pomoni ukumbini hapo
kushuhudia burudani ambayo pia ilishuhudiwa na mwimbaji wa bendi ya
Mapacha Watatu, Kalala Hamza 'Junior', Meneja wake, Hamisi Dacorta na
wanamuziki wengine wa FM Academia, Patcho Mwamba na Pablo Masai.
Waimbaji
wa Twanga Pepeta, Ramadhan Athuman 'Dogo Rama', Venance Mgori na rapa
na mwimbaji, Jumanne Said, wakiongozwa na kiongozi msaidizi wa bendi
hiyo, Saleh Kupaza, walidhihirisha hakuna pengo lililoachwa na Chaz
Baba kutokana na kuimba kwa ufasaha, 'vipande' alivyokuwa akiimba.
Wanamuziki
wengine wa Twanga Pepeta waliokuwa jukwaani kuongoza mashambulizi ni
kiongozi mkuu, Luiza Mbutu, Amigolas, Haji Ramadhan (mshindi wa BSS
2011), Mwinjuma Muumin, Janeth Isinika, Khadija Mnoga 'Kimobitel',
Grayson Semsekwa na Msafiri Said 'Diouf'.
Pia
walikuwepo wapiga vyombo, Miraji Shakashia 'Shakazulu', Jojoo Jumanne,
Godfrey Kanuti, Selemani Shaibu, Victor Nkambi na Hassan Kado.
Wanenguaji ni Asha Said 'Sharapova', Maria Soloma, Betty Johnson 'Baby
Tall', Mary Khamis na wengineo.
Twanga
Pepeta hivi sasa inatamba na albamu yake ya 11 ya Dunia Daraja yenye
nyimbo za Kauli, Kiapo cha Mapenzi, Umenivika Umasikini, Mtoto wa
Mwisho, Dunia Daraja na Penzi la Shemeji.
Albamu
zilizopita za bendi hiyo ni Kisa cha Mpemba (1999), Jirani (2000),
Fainali Uzeeni (2001), Chuki Binafsi (2002), Ukubwa Jiwe (2003), Mtu
Pesa (2004), Safari 2005 (2005), Password (2006), Mtaa wa Kwanza (2007)
na Mwana Dar es Salaam (2009).
No comments:
Post a Comment